Siku ya leo nataka tujifunze kutoka kwa tai. Kuna mengi ya kujifunza Kutoka kwa tai ila kwa leo acha twende na hili.
Tai akitaka kumla nyoka anamnyanyua kwa nguvu na kwa spidi kali ambayo nyoka hawezi kuhimili mpaka juu, Kisha anamwachia.
Nyoka akiwa bado hajaelewa kinachoendelea tai anamdaka haraka kabla hajadondoka chini na kupanda naye juu zaidi katika mazingira ambapo tai anajisikia huru kufanya chochote.
Kisha anamrarua nyoka…
Anaweza kufanya hivyo kwa nyoka yeyote bila kujali ukubwa wa nyoka husika.
SOMO: Kila mtu ana eneo lake la kujidai. Kwa tai eneo lake la kujidai Ni huko angani. Akipigana na nyoka wakiwa ardhini, lazima tu atafeli, ila akimchukua juu nyoka hana ujanja.
Wewe pia unapaswa kufahamu eneo lako la kujidai. Kisha litumie kwa manufaa yako.
SOMA ZAIDI:
Kupata ebooks nzuri za kusoma BONYEZA HAPA
2 responses to “Tai Anatufundisha Somo Hili Kubwa Kuhusu Maisha Ya Mafanikio”
Every one indeed is unique, but we normally fail to know ourselves.
Bigup Bro. You really inspires me alot.
[…] Tai Anatufundisha Somo Hili Kubwa Kuhusu Maisha Ya Mafanikio […]