Ungekuwa wewe umewekeza kwenye hii kampuni ungefanyaje?


Brown Unaendeleaje? Bila shaka umeamka salama  kabisa.

Leo ninataka niongee na wewe kuhusu uwekezaji.

Kwanza ebu niambie mimi, Ni kampuni gani unaikubali hapa Tanzania? Ni kampuni gani ambayo kwa vyovyote vile unapenda  huduma zake na kamwe huchoki kwenda kwao. Ebu niambie ni ipi hiyo?

Inaweza hata isiwe kampuni kubwa, ikawa biashara yoyote ya kawaida tu, pengine hata mtaani kwako, ila wewe binafsi unaikubali. Kila mara lazima uende kwao kupata huduma zao.

Sasa ebu fikiria kwa jinsi ambavyo wewe unaikubali hiyo kampuni, biashara au taasisi hiyo, ungekuwa wewe ndiye mmiliki au mmoja wa watu wenye maamuzi makubwa kwenye hiyo kampuni ni kitu gani cha ziada ungefanya kuhakikisha kwamba kampuni yako inazidi kusongambele?

Ebu andika jibu lako chini. Ujue jibu lolote utakalopata litakusaidia wewe pia.

Nataka jibu lolote utakalopata uende na wewe ullitumie kwenye biashara au kipaji chako.

Kama  umeona hicho kitu ndicho kinaweza kuifanya biashara unayoikubali bora zaidi, na wewe ukikitumia ni wazi kuwa kitaboresha biashara yako pia. Kwa hiyo kakitumie wewe KWENYE kampuni au biashara yako.

Pia tumia mbinu nyingine ambazo unaziona kwa hiyohiyo kampuni unayoikubali.  Angalia mbinu ambazo wanatumia kuhudumia wateja, kuwasiliana nao n.k.

ZITUMIE kuboresha biashara yako na kuifanya kuwa Bora zaidi.

Kama unaikubali biashara hiyo kwa sababu ya huduma nzuri. Na wewe Anza kutoa huduma nzuri Kama wao wanavyofanya. Iga kwao. Inashangaza kuona kwamba watu huoenda kuiga vibaya na kuacha sifa nzuri kama hizi. Sasa ebu wewe ziige hizi sifa.

Muda siyo mrefu utaweza kuifikisha mbali sana hiyo biashara yako.

Kama unaikubali biashara au kampuni hiyo kwa sababu ya bidhaa Bora, ebu na wewe anza kuzalisha bidhaa Bora.

Kwa vyovyote vile. Endelea kusonga mbele. Utaweza kufanya makubwa zaidi pale utakapokuwa na mtu unayemwangalia na kujifunza masomo kwake. Ukajifunza na kufanyia kazi unachojifunza.

Kila la kheri.

Godius Rweyongeza
Morogoro-Tz
0755848391
https://songambele.co.tz


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X