Kuna mtu unaweza kumkuta anatafuta wazo la biashara ambalo halijawahi kufanyika, kitu ambacho hakijawahi kuonekana
Kiufupi wazo la aina hii halipo. Hata ukiangalia biashara kubwa zilizopo leo hii, hakuna biashara mpya.
Wazo la kuanzisha Google siyo jipya. Isipokuwa Google wameboresha na kurahisisha utafutaji wa habari. Ila tangu zamani babu zetu walikuwa wakipashana habari kwa mdomo,
Tofauti ya sasa na siku zile ni uharaka. Wa upatikanaji wa taarifa.
Ndiyo maana nakwambia huhitaji wazo la biashara ambalo halijawahi kufanyika.
Na hata imitokea ukapata wazo la aina hii, fahamu kuwa siyo tu wewe utakayefanya biashara hiyo peke yako. Kanuni ya copy cut inasema:
Ukianzisha biashara yako, ndani ya miezi sita, Kuna watu wengine watakuwa wameanzisha biashara ya aina hiyo.
Hivyo badala ya kupambana kupata wazo ambalo halijawahi kuwepo, boresha mawazo yaliyopo sasa.
Amazon walianza kwa kuuza vitabu, hawakugundua kitu kipya waliboresha kilichokuwepo na kukiweka mtandaoni. Uuzaji wa vitabu umekuwepo kwa muda mrefu. Amazon waliboresha uuzwaji tu.
Kiufupi katika ulimwengu wa sasa, kama una wazo la biashara au Kama kuna kitu kinafanyika, kiweke mtandaoni.
Warahisishie watu utumaji na upokeaji wa fedha
Warahisishie watu njia za usafiri
Warahisishie watu upatikanaji wa chakula.
Siku ya leo angalia wazo gani ambalo lipo, ambalo unaweza kulirahisisha na kuliweka mtandaoni
2 responses to “WAZO LA BIASHARA AINA HII LAHUWEZI KULIPATA”
Huko sahihi Sana mkuu, nimejifunza kupitia SoMo hili, Kwan hakuna biashara mpys kikubwa ubunifu ndiyo unaitajika zaidi
[…] makala iliyopita nilikwambia kwamba huwezi kupata wazo la kipakee la biashara. Ni vigumu kupata wazo ambalo halijawahi kufanyika […]