1. Usisahau kuweka AKIBA. Kwa kila kipato chako unacjopata weka akiba ya asilimia 10.
2. Usitumie fedha zaidi ya unavyoingiza.
3. Usifanye vitu kuwaridhisha watu.
4. Usitegemee chanzo kimoja cha kipato na hasa mshahara.
5. Mara zote kuwa na kitabu na soma vitabu.
6. Hakikisha unakuwa na malengo na unayafanyia kazi.
7. Ukitaka kuibadili dunia. Anza kufanyia mbele ya nyumba yako. Ukitaka kuibadili dunia tandika kitanda.
8. Usiangalie runinga na hasa taarifa ya habari.
9. Usisahau kuwa maisha ni wajibu wako. Ukishinda ni juu yako na ukishindwa ni juu yako.
10. Mahusiano yako yawe kipaumbele kwako.
Kwa sasa kutoka hapa mji kasoro bahari; mji kasoro pwani sina la ziada.
Umekuwa nami,
Godius Rweyongeza
0755848391
Morogoro-Tz
One response to “Hata kama itatokea ukasahau vyote maishani, Ila hakikisha hausahau kufanya hivi vitu”
kwanini tusiangalie runinga na hasa taarifa ya habari, nieleweshe hapo kaka