Jinsi Ya Kulipwa Kwa Kufanya Kile Unachopenda


Unaendeleaje rafiki yangu.

Leo ni siku ya kipekee sana. binafsi nimeona nije kwako kwa lengo la kukueleza kitu kidogo tu, namna ambavyo wewe unawezakulipwa kwa kufaya kitu unachopenda.

Zamani mambo yalikuwa shaghalabaghala. Ulikuwa unatakiwa kusoma kozi fulani na baadaye kwenda kufanya kufanya kazi hata kama kozi au sekta husika ulikuwa huipendi. Ila leo hii mambo yamebadilika, kuna njia mpya za kukusaidia wewe kufanya kile unachopenda na hata ukaweza kulipwa kwa hicho kitu.

Labda kwanza nikuulize wewe, ni kitu gani ambacho unapenda kufanya maishani mwako? Ni kitu gani ambacho haipiti siku bila ya wewe kukifanya? Ni kitu gani hicho?

Nimeshuhudia watu wakilipwa kwa vile vitu wanavyofanya kuanzia kwa waangalia tamthiliya, wasoma vitabu, wapenzi wa mpira, waandishi, public spkeakers, walimu, watafiti n.k.

Ngoja nikuulize tena, wewe ni kitu gani ambacho unapenda kufanya kutoka moyoni? Je, ungependa kulipwa kwa kufanya hicho kitu. Basi kaa mkao wa kula

Kama wewe ni mpennzi wa kusoma vitabu, siku za nyuma nilishaelez namna ambavyo unaweza kulipwa kwa kusoma vitabu hapa.

Hakikisha umeangalia video hii youtube: imeeleza mbinu za kulipwa kwa kusoma vitabu

Kwa ambao wanapendelea kufanya vitu vingine tuendelee mbele.

Kwanza ukishajua ni kitu gani ambacho unapenda, unapaswa kwenda hatua ya ziada na kuanza kufanya kile kitu hata kama ni kwa udogo. Anza kufanya kile kile na washirikishe watu wajue kwamba wewe ni mtaalamu kwenye hicho kitu.Aanza kujenga hadhira ya watu ambao wanafuatilia kazi zako.

Kama unapenda kuimba, anza kuimba.

Kama unapenda kuchora,  chora.

Kama unapenda kuandika andika.

Kiufupi kwa chochote kile unachopenda kukifanya basi hakikisha kwamba unatafuta namna ya kuwafanya watu wajue kwamba unachopenda kufanya kutoka moyoni ni hicho.

Na njia nzuri ya kuwaambia watu ni kwa wewe kufanya na kuweka kwenye vitendo kile unachopenda.

Unaweza kufanya hivyo kwa kurekodi video na kuwashirikisha au kwa kuandika makala au kwa kuchora na kuweka michorao yako mtandaoni.

Hii ni hatua ya kwanza ambapo utajitambulisha kwa watu na watu wataanza kujua kwamba upo.

Hatua ya pili ni kuhakikisha kwamba unaanza kujenga timu ya wafuasi kindakindaki. Kwenye wale wafuasi wako, kuna wale ambao watakuwa wanapenda kufuatilia kazi zako kwa ukaribu zaidi. Yaani, wale watakaokuwa wanapenda kufuatilia kazi zako kiasi kwamba ikitokea ukakaa kimya kwa siku mbili au tatu kabla hujatoa kazi zako kulingana na utaratibu wako watakupigia mpaka simu kujua kuna kitu gani ambacho kinaendelea.

Kama unatoa mafunzo kwa  njia ya video au sauti, kuna watu watakuwa wanafuatilia kazi zako kiasi kwamba ikipita siku moja au mbili ukiwa hujatoa kazi yako watahoji kwa kutuma jumbe fupi au hata kupiga simu.

Hawa ni watu wachache ambao unawahitaji kwenye safari yako.

TATU, jiwekee utaratibu wa kuwa unatoa kazi zako. unapaswa kuwa na utaratibu maalumu wa kutoa kazi zako, kama unatoa kazi zako mara moja kwa wiki au kila siku, hakikisha kwamba unafanya. mfano mimi ukija hapa kwenye hii blogu, ni lazima tu  kila siku zitawekwa makala mbili mpya. kila siku. Sasa na wewe tengeneza kijiutaratibu chako na kifuate.

Nne angalia ni namna gani unaweza kutengeneza bidhaa inayoendana na wafuasi wako.

Kama utafuata hatua ya kwanza na pili vizuri, hatua ya nne ni rahisi sana, hasa kwenye ulimwengu wa leo. Kadiri utakavyokuwa ukifanya kile kitu unachofanya, kuna watu watajitokeza kwa kuuliza maswali. Haya maswali unayoulizwa, kuwa makini nayo, maana hizi ndizo dukuduku ambazo zinawasumbua watu. sasa na bidhaa zako hazipaswi kwenda mbali sana na hizi dukuduku. Hivyo unaweza kutengeneza bidhaa au huduma katika namna ya kujibu hayo maswali.

Tano, uza bidhaa uliyotengeneza kutokana na dukuduku au tatizo linalowakumba watu. Kwa kuwa ulishawasoma watu tangu mwanzo, sasa kifuatacho ni wewe kuanza kuwapa huduma au kitu ambacho walikuwa wanauhitaji wao. Kile ambacho wao walikuwa wanakuuliza mara kwa mara.

Na hapa kwenye kuuza kuna watu ambao wataanza kukwambia kwamba haupaswi kuuza kitu chochote, badala yake huduma zako zote zinapaswa kuwa bure. Ila siyo kweli, kuna huduma ambazo watu wanapaswa kulipia na kuna huduma za bure. Kama ni huduma za kulipia, basi ziwe za kulipia kweli ili zikuwezeshe wewe kujikimu na kuweza kuendelea kutoa huduma nyingine zaidi.

Mimi ukija hapa kwenye blogu, utakutana na makala mbili za kukuelimisha wewe kila siku. Huzilipii chochote, lakini pale ninapoandika kitabu, basi utatoa kiasi kidogo kupata kitabu au kozi husika.

Nashauri pia usome ebook ya KIPAJI NI DHAHABU. Ina mengi ya kukusaidia wewe kwenye kujenga kipaji chako, kukikuza na kukiendeleza. Baada ya kusema hayo, naomba nikutakie kila la kheri.

KIPAJI NI DHAHABU: Jinsi Ya Kukigundua, Kukinoa Na Kutumia Kipaji Chako Kwa Manufaa

NB. Nashauri sana uhakikishe kwamba kazi zako ni za viwango mara zote.

Ni mimi

Godius Rweyongeza

0755848391

Morogoro-Tz


One response to “Jinsi Ya Kulipwa Kwa Kufanya Kile Unachopenda”

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X