Jinsi Ya Kutatua Changamoto Unazokutana Nazo


Habari ya siku hii njema sana rafiki yangu wa ukweli. Leo ni siku nyingine ya kipekee sana na leo nataka nikwambie kwamba usikubali kamwe kwenye maisha yako changamoto zikuzuidi wewe kukufanya ushindwe kufanikisha malengo yako.

Siku zote changamoto huwa zinatokea. Changamoto ni kama zinatokea kukuonesha kwamba je, uko siriazi kweli na kile kitu ambacho unataka. Sasa kama hauko seriazi ndio utakuta kwamba unataka tamaa na kuishia njiani. Ila kama kweli uko siriazi utapambana kuhakikisha kwamba unaitatua hiyo changamoto na kuendelea mbele.

Kitu muhimu unachopaswa kufahamu ni kwamba hauko peke yako mwenye changamoto. Wakiitwa watu wote hapa na wakaambiwa kwamba waweke changamoto zao hapo mezani halafu mgawane hizo changamoto, utakuta kwamba changamoto za kwako ni ndogo sana kuliko za hao watu wengine. Kuna watu wana changamoto kubwa kuliko wewe. Hivyo basi kitu kimoja ambacho ninaweza kukushauri hapo rafiki yangu ni kwamba jitahidi upambane na hali yako mpaka kieleweke. Kamwe, usikate tamaa kwenye kutatua changamoto au kufanyia kazi changamoto ambazo zinatokea maishani mwako.

Upo level gani kwenye kutatua changamoto

Hivi umewahi kujua kuwa kuna level za kutatua changamoto? Kama ulikuwa hujui basi kaa chini ili nikujuze rafiki yangu. Changamoto zina viwango bana. Ukiona kwamba umekutana na changamoto na imekushinda wewe kuitatua, basi ujue kwamba changamoto hiyo ina nguvu kubwa kuliko wewe.

Binafsi huwa napenda kuziweka changamnoto kwenye mstari wenye namba moja mpaka kumi. Wewe ukikutana na changamoto ambayo ni kubwa kuliko wewe, maana yake lazima utaka tamaa na kuishia njiani na kuona kama vile hakuna maisha baada ya hapo.

Ila kama wewe ni mkubwa kuliko changamoto, ukikutana na changamoto ambayo umeizidi kwako, itakuwa ni rahisi kuitatua. Hivyo, basi unapaswa kuwa makini kwenye kufanyia kazi changamoto kwenye maisha yako.

Ukikutana na changamoto kubwa, tuseme changamoto namba 7 na wewe uko kwenye viwango vya namba 5 ni wazi kuwa hiyo changamoto utaikimbia tu. Ila kama wewe uko kwenye viwango vya namba 9 kwenye kutatua changamoto na ukakutana na changamoto namba 7 ni wazi kuwa hiyo changamoto kwako itakuwa ni rahisi sana.

Jijengeea uwezo wak utatua changamoto. Hiki ni kitu muhimu sana. Unapaswa kujijenea uwezo wa kutatua changamoto. Ukikutana na changamoto, usizikimbie, kuwa tayari kuzifanyia kazi mpaka utoboe.l changamoto ni sehemu ya maisha tu. Hivyo, kuwa tayari kuzifanyia kazi.

Changamoto huwa haziishi. Njia pekee ya wewe kumaliza changamoto ni wewe kuwa mkubwa kuliko changamoto zenyewe. na kamwe usije ukakimbia changamoto uliyokutana nayo.

Kila la kheri

Umekuwa nami rafiki yako wa ukweli

Godius Rweyongeza

,

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X