Jinsi Ya Kutoa Na Kupokea Mrejesho


Mrejesho ni miongoni mwa ujuzi muhimu sana unaopaswa kuwa nao.  Aidha iwe ni kutoa au kupokea mrejesho.

Mrejesho ni kutoa au kupokea mapendekezo ya kumsaidia mtu kuboresha kazi yake.

Kuwa mtu wa kupokea mrejesho na kuufanyia kazi na hasa pale unapokuwa na mrejesho unaoona kabisa kwamba unaenda kuwa mrejesho wenye manufaa kwako.

Kwetu sisi kutoa mrejesho kwa watu wengine huwa tunaona ni Jambo la kawaida sana

Kwa mfano kusema kwamba kocha wa timu ya Simba alipaswa kumweka mchezaji fulani uwanjani, inakuwa ni rahisi sana kwetu kusema hivyo.

Ila wewe ukipewa mrejesho unakuta kwamba inakuwa ngumu, kwako kupokea mrejesho.

Mrejesho unakufanya unaimarika.
Siku nyingine ukiandika kitabu, mpe rafiki yako akisome; Ila mpe ambaye unajua atakupa mrejsho baada ya kukisoma.

Ukiwa na logo ya biashara au kampuni unaweza kumpa mtu ili akupe mrejesho baada ya kuiona logo yako.

Unaweza kuomba mrejesho wa kukusaidia wewe kutatua tatizo

Mrejesho pia unaweza kuwa wa maoni ya mtalaam.

Lakini pia mrejesho unaweza kuwa ni kwa ajili ya kupata maoni ya mtu mwingine mwenye mtazamo tofauti au anayetokea eneo la tofauti na unapotokea. Na hapa simaanishi kwamba kama wewe kwenu ni Tanga basi umpe mtu wa Mtwara, Bali kuwa kama wewe ni mwanasheria basi mpe daktari akupe mrejesho. Huyu atakupa mtazamo wa kidakatari kwenye kazi yako na hivyo kuiboresha.

Kama wewe wewe ni mwalimu mpe mhandishi akupe mrejesho. Hapo utakuwa umepata mrejesho kutoka kwa mtu mwenye mtazamo tofauti na wewe.

Mrejesho unaweza kutolewa kwako kwa njia ya sauti, video au maandishi

Asante sana rafiki yangu.
Umekuwa nami rafiki yako wa ukweli
GODIUS RWEYONGEZA
0755848391
MOROGORO-TZ


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X