Kafanyaje huyu?


Kapata pressure baada ya biashara yake kutofanya vizuri!

Tafiti zinaonesha kuwa Kati ya biashara 10  zinazoanzishwa biashara tano hufa ndani ya mwaka mmoja na nyingine ambazo hubaki huwa hazifikishi miaka 10.

Hili wewe mwenyewe lifuatilie mtaani kwako. Utakuta kwamba kuna biashara nyingi zinazoanzishwa  baada ya muda kidogo zinapotea.

Hii ndio kusema kwamba usipokuwa makini wakati unaanzisha biashara, utajikuta kwamba na wewe unakuwa miongoni mwa hizo takwimu za biashara kufa ndani ya mwaka.

Sasa yafutayo ni mambo muhimu ya KUZINGATIA Unapokuwa unafanya biashara.

Hakikisha biashara yako inakuwa kipaumbele kwako. Yaani, biashara yako itunze kama unavyomtunza mtoto mchanga.

Kila mwezi mtoto anapelekwa kliniki ili kupimwa baadhi ya vipimo.

Wewe pia kila mwezi ipime biashara yako. Pima mauzo yako. Mtaji unaozunguka. Pima mauzo yaliyofanyika na wateja walionunua pamoja na masoko yaliyofanyika ikiwa ni pamoja na matokeo ya masoko.

Kitu hiki kidogo kitakupa mwongozo wa biashara ilipotoka na inapoelekea. Na utaepuka biashara yako kufa ndani ya mwaka mmoja.

Pata kitabu changu cha MAMBO 55 YA KUZINGATIA KABLA KUANZISHA BIASHARA. Utajifunza mengi ya kukusaidia kuanzisha na kukuza biashara yako. Kitabu hiki ni ebook na kinapatikana kwa elfu 5 tu. Rusha elfu 5 kwa 0755848391 jina ni GODIUS RWEYONGEZA


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X