KITABU:MAAJABU YA KUWEKA AKIBA: Jinsi Tabia ya Kuweka Akiba Inaweza Kukufanya Uwe Tajiri


Mwaka juzi (2020) niliandika kitabu cha MAAJABU YA KUWEKA AKIBA. Kwenye kitabu hiki niliandikabutangulizi huu hapq chini ambao Leo hii bado una nguvu kubwa aawa na nilipouandika.

“Tangu umezaliwa mpaka leo hii, ni unaposhika kitabu hiki mikononi mwako ni wazi kuwa fedha nyingi tayari zimepita mikononi mwako. Hivi laiti ungekuwa umeweka utaratibu wa kuwa unatoa kiasi kidogo kwenye kile ambacho unapokea na kukiweka kama akiba, unadhani leo hii ungekuwa na kiasi gani?

Niliwahi kumwuliza dada mmoja swali hili hapa, akawa amefikiri kwa muda, kisha akaniambia, “Loo! Ningekuwa na fedha nyingi sana”. Bila shaka na wewe utakuwa na majibu kama hayo ambayo huyo dada alikuwa nayo.

Kila mtu huwa anapokea fedha kwa viwango tofauti, japo kiasi ambacho unapokea sasa hivi kinaweza kuonekana kidogo. Lakini ukiweka utaratibu wa kuweka akiba kutoka kwenye hicho kidogo, ni wazi kuwa itafikia hatua ambapo hicho kidogo kitakuwa kikubwa.

Ni imani yangu kuwa baada ya kuwa umesoma kitabu hiki hapa, utachukuka hatua na kuanza kuweka akiba bila ya kuchelewa. Nipo nafikiri tu kuwa kwa mfano, ukimfundisha mtoto wako misingi ambayo utajifunza humu ni wazi kuwa mpaka anakuja kufikisha miaka 18 au 20 basi atakuwa ameweka akiba ya kutosha kumfanya hata aweze kujilipia ada ya chuo kikuu bila kuhitaji mkopo wa chuo. Na kwa sababu atakuwa amejenga msingi imara basi ni wazi kuwa bado kiasi zaidi kitakuwa kinazidi kuingia kwake.”

Rafiki yangu hayo ndiyo maneno kuntu niliyoandika mwaka 2022. Leo hii nimeguswa na umuhimu wa maneno haya kiasi kwamba, nikaona nitalete kwako. Yasome na uyaweke kwenye vitendo. Kikubwa zaidi hakikisha UMESOMA KITABU CHA MAAJABU YA KUWEKA AKIBA. Kinapatikana kwa elfu 5 tu na Ni softcopy.

Tuma fedha kwa namba 0755848391 jina Ni GODIUS RWEYONGEZA


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X