Ninataka nikwambie kitu kitakachobadili maisha yako kuanzia leo hii na kuendelea.
Nataka ufanye zoezi hili rahisi sana.
Anza kwa kujiuliza vitu na shughuli zako zote unazofanya.
Sasa angalia ni shughuli ipi ambayo ukiacha kuifanya na KUWEKEZA nguvu zako kwenye shughuli zinazobaki utapata matokeo makubwa sana.
Kama ipo achana nayo. Kisha nguvu zako na muda wako uwekeze kwenye hizi shughuli nyingine ambazo zitakupa matokeo makubwa.
Kuna kanuni inaitwa kanuni ya 80/20
Kadiri ya kanuni hii ni kwamba asilimia 80 ya matokeo unayopata yanatokana na shughuli kidogo unazofanya ambazo ni sawa na asilimia 20.
Kwa hiyo kama kila siku unajishughukisha na majukumu 10, ni majukumu mawili tu ambayo yanakupa matokeo makubwa.
Kama kama Kuna kazi nyingi zinazokuingizia kipato, unapaswa kukaa chini na kutafakari. Kuna kazi chache zinazoingiza kipato zaidi. Ukiwekeza nguvu zaidi kwenye hizo chache utapata matokeo makubwa zaidi. Na hii ndio dhana nzima ninayotaka utumie kuanzia leo hii.
Kila la kheri
Umekuwa nami .
Rafiki yako wa ukweli Godius Rweyongeza
0755848391
Morogoro-Tz
One response to “Kitu Kitakachobadili maisha yako leo hii na hata milele”
Very helpful