Kitu gani unaenda kufanya wiki hii ili kujisogeza karibu na malengo yako?


Kwenye kitabu changu cha KUTOKA SIFURI MPAKA KILELENI, nimeeleza kwamba kadiri unavyokuwa unafanyia malengo yako, yenyewe yanakuwa yanasogea karibu pia. Hivyo, Kuna sehemu mtakutana ambayo ndiyo pointi ya wewe kufikia melengo yako.

Sasa wiki mpya tayari imeanza, ni kitu gani unaenda kufanya wiki hii ili usogee karibu na malengo yako?

Hakikisha unafanya kitu. Bila kufanya kitu unaweza kuishia kusema labda Mimi nimerogwa au nimelaaniwa, Ila kumbe siyo.

Unaweza kusema Mungu hajanibariki, lakini kumbe hajaona juhudi zako ili akubariki. Si unajua Mungu anabariki juhudi eeh!

Haya Sasa kazi ni kwako. Kwenye mipango yako ya wiki hii, chagua kitu kimoja ambacho utafanya. Kisha komaa nacho mpaka kieleweke. Kila la kheri.

Godius Rweyongeza
0755848391
Morogoro-Tz


One response to “Kitu gani unaenda kufanya wiki hii ili kujisogeza karibu na malengo yako?”

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X