Namna ya kufanya usomaji wa vitabu uwe sehemu ya pili ya maisha yako


Kusoma ni tabia. Na tabia yoyote hujengwa.  Kuna tabia ambazo unazo sasa hivi unazifanya ila hujiulizi mara mbili kama uzifanye au uache. Kwa mfano kila siku unapiga mswaki ila hujiulizi mara mbili kwamba upige au usipige leo utapiga mswaki kesho. Yaani, kupiga mswaki kumeshakuwa tabia yako ya pili.

Sasa hata kusoma kunapaswa kuwa tabia yako ambayo unafanya bila kujiuliza. Na unaweza kuifanya iwe tabia yako ya pili kama utaamua kila siku kusoma kitu. Yaani, hakikisha ukianza leo kusoma na kesho soma. Na kesho kutwa soma pia. Hivyo ndivyo utajenga tabia ya kusoma kila siku.

Robin Sharma kwenye kitabu chake cha The 5am Club anasema kwamba tabia ya kweli inajengwa ndani ya siku 66. Yaani siku 22 za mwanzo zinakuwa ni kuanzisha tabia. Siku hizi huanza vizuri kabisa ila huanza kuwa ngumu katikati. Siku 22 zinazofuata huwa ngumu zaidi ila ukizivuka hizi utakuwa umeimarika sana. Siku 22 za mwisho ndio tabia yako inakuwa tayari imejengeka. Kwa  hiyo na wewe kuanzia leo weka mpango wa kusoma kitabu kila siku kwa siku 66 bila kukosa. Itapendeza zaidi kama muda huo wa kusoma utakuwa ni ule ule kila siku.


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X