Ndoto siyo ile unayoota ukiwa umelala, ndoto ni ile unayoona ukiwa macho


Kama kuna kitu ambacho utapaswa kufanya maishani mwako na kikawa ni kitu chenye manufaa makubwa kwako ni kukaa chini na kuandika ndoto yako chini. Unaweza kuona kukaa chini kupanga vitu ambavyo ungependa kufikia maishani mwako kama ujinga, ila ukweli ni kwamba ukishindwa kupanga unakuwa unapanga kushindwa. Kiuhalisia muda ambao unatumia kupangani mdogo ukilinganisha na manufaa unayopata baadaye. Unaweza kutumia saa moja asubuhi kupangilia siku yako, ila sasa hilo likakufanya ufanikishe makubwa na wakati huohuo ukaepusha mambo mengine ambayo yangeweza kutokea kinyume na matarajio.

Unaweza kutumia wiki moja kupangilia juu ya mwaka wako, ila hiyo wiki utakayoitumia ikakufanya uokoe mwaka wako. Kwa hiyo, usiogope kukaa chini na kupanga. Unapaswa kuwa na ramani kamili ya wapi ungependa kufika baada ya mwaka, baada ya miaka mitano, kumi, ishirini na hata zaidi. kiufupi linapokuja kwenye suala zima la kupanga weka mipango yako kama vile utaishi milele ila ifanyie kazi mipango yako leo kama vile hii ndio siku yako ya mwisho.

Kazi ya kufanya wiki hii:

Kaa chini na upangilie mambo ambayo ungependa kufanikisha baada ya miaka 20, kumi, mitano na mwaka mmoja.

Kisha panga malengo ambayo utayafanyia kazi mwezi huu, wiki hii na leo hii n.k.

Kumbuka kupanga muda wa wewe kwenda kupangilia ndoto zako za miaka 5, 10, 30 n.k. ni sehemu ya mpango unaopaswa kuuweka. Hivyo, chukua hatua sasa.


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X