Bidhaa mbalimbali huwa zinatambulika kwa majina. Kila mtu huwa anatambulika kwa jina lake. Hata hivyo iko wazi kuwa baadhi ya majina yakitajwa, yanakuwa na nguvu ukilinganisha na majina mengine.
Kuna kampuni ikizindua bidhaa fulani, watu wataikimbilia kuinunua na kampuni nyingine inaweza kuzindua bidhaa ya aina hiyohiyo ila watu wakawa hawajaikimbilia. Na ukifuatilia kiudani zaidi unaweza kugundua kuwa kilichowafanya watu waende kununua bidhaa kwenye kampuni A badala ya kampuni B, unakuta sio ubora wa bidhaa bali ni jina.
Kitu kama hiki hapa tunaweza kukiona kwenye zama hizi hapa. Kwa mfano, kuna watu wanakimbilia kununua simu za aina fulani sio kwa sababu ya ubora wake, ila kwa sababu ya jina lake. na wengine wanahakikisha kwamba wana bidhaa zote za kampuni husika bila kubakiza hata moja. Utasikia mtu anakwambia kwamba mimi kampuni fulani ikitengeneza bidhaa yoyote ile lazima tu niinunue tu. Kinachomsukuma ni JINA.
Asikudanganye mtu, jina lina linaweza kukufanya uuze au usiuze. Jina linaweza kukufanya upokelewe vizuri sehemu fulani au usipokelewe.
Kitu muhimu cha kufahamu ni kuwa, watu wananunua jina. Kama huamini toa wiki moja ambayo utaenda kwa watu ukijitambulisha kama YUDA ISIKARIOTI, halafu uone jinsi watu watakavyoupokea huo utambulisho wako!
Pale utakapotakiwa kuchagua jina la biashara yako, kampuni, bidhaa au hata tovuti yako mtandaoni, usikurupuke tu kutoa jina. Jipe muda wa kufikiri kwa kina ili upate jina ambalo ni zuri. Wahaya wana methali inyosema kuwa eibara libi, liita nyinalyo. Ikimaanisha jina baya huua mtoaji wa jina hilo.
Kwa hiyo, kama unataka kuua bidhaa yako au biashara yako toa jina baya na kama unataka kuijenga biashara yako ipe jina zuri. Kwenye kitabu changu cha Mambo 55 Ya Kuzingatia Kabla Ya Kuanzisha Biashara, nimeeleza kiundani juu ya hatua za kuchukua kwenye kupata jina bora la biashara yako. Tuma elfu tano kwa 0755848391 kupataa kitabu hicho.
4 responses to “Nguvu Ya Jina (jina la biashara, jina lako na Jina la brand yako)”
Well stated
Really Nakubali kaka Big up
Kitabu chicho Ni soft copy au hard copy
Hardcopy na softcopy