Kama kuna mtu ambaye amekufikisha wewe juu, mtu huyohuyo anaweza kukuangusha chini.
Kama umetumia njia ya mkato, njia hiyohiyo inaweza kukurudisha chini
Njia nzuri na ya pekee ya kupata matokeo yadumuyo ni kufuata mchakato.
Mchakato unakujenga.
Hata ukianguka unaweza kusimama tena maana unakuwa unaujua mchakato. Rafiki yangu, kazana kuujua mchakato, kisha ufuate.