Njia Tano Rahisi Za Kukuza Biashara Kwenye Zama Hizi Za Mtandao


Rafiki yangu hongera sana kwa siku hii nyingine na ya kipekee sana. Siku ya leo ningependa nikuelekeze njia tano tu ambazo zitakusaidia wewe kukuza biashara yako kwenye zama hizi za intaneti. Njia hizi ni rahisi kufanyika na unaweza kuzifanyia kazi popote pale ulipo

Kwanza hakikisha kwamba biashara yako ipo kwenye mtandao. Kwenye zama hizi hapa mtu akitaka kitu, sehemu ya kwanza kabisa ambapo anakimbilia ni mtandaoni, hivyo ni jukumu lako kuhakikisha kwamba na wewe unaiweka biashara yako mtandaoni ili watu wakiingia mtandaoni wanatafuta kitu waweze kuikuta. Watu wanapaswa kuikuta biashara yako mtandaoni,  na njia rahisi ya watu kuikuta biashara yako mtandaoni ni kwa wewe kuhakikisha kwamba

  • Umefungua blogu au tovuti ambapo watu wakitafuta kitu watakukuta tayari ukiwa una kitu ambacho unaweka
  • Kuwa na akaunti ya google my business.
  • Kuwa na akaunti za mitandao ya kijamii na kuhakikisha kwamba unazitumia vilivyo
  • Kuwa na namba ya simu ya biashara na kuhakikisha kwamba unaitumia vilivyo kwa kutunza mawasiliano ya wateja wako na kuhakikisha kwamba wateja wako wanawasiliana na wewe kupitia namba hiyo.
  • Ikumbukwe kuwa namba ya biashara siyo namba ya simu binafsi.

Rafiki yangu, hizo hapo ndio njia ambazo unaweza kutumia kuhgakikisha unakuza biashara yako hasa kwenye zama hizi hapa.

Kila la kheri.

Ni mimi rafiki yako wa ukweli Godius Rweyongeza


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X