UWEKEZAJI NI NINI?


Moja ya eneo ambalo limekuwa halieleweki miongoni kwa watu wengi basi ni UWEKEZAJI.

Kumekuwepo na dhana mbalimbali kuhusu UWEKEZAJI na WAWEKEZAJI. Hizi dhana zimewafanya watu wengi washindwe KUWEKEZA huku wachache wanaoilewa dhana hii wakiwa wanawekeza kwenye maeneo ya muhimu kwa manufaa makubwa.

Dhana potofu kuhusu UWEKEZAJI.

Kumekuwepo na dhana mbalimbali kuhusu UWEKEZAJI. Na moja ya dhana kubwa  ambayo imekaa kwenye vichwa vya watu wengi ni dhana kuwa mwekezaji ni mtu wa nje. Fungulia redio au runinga, kila utakaposikia wakizungumzia kuhusu UWEKEZAJI au MWEKEZAJI basi wanakuwa wanamwongelea mtu wa kigeni.

Hiki kitu kimemfanya watu wengi waamini kwamba mtanzania hawezi kuwa mwekezaji. Au kiufupi tu kuwa kama wewe siyo mtu kutoka nchi za nje basi basi wewe siyo MWEKEZAJI. Au labda nikuulize wewe, ni mara ngapi umeona au kusikia watanzania wakijiita wawekezaji?

Hata hivyo, ifahamike kuwa siyo kwamba mtanzania hawezi kuwa mwekezaji. Wewe mwenyewe unaweza kuwa mwekezaji mzuri tu.

MWEKEZAJI anapaswa kuwa na fedha nyingi

Dhana nyingine kuhusu uwekezaji ni kwamba mwekezaji anapaswa kuwa na fedha nyingi. Nenda kaongee na mtu yeyote unayemfahamu na ongelea kuhusu UWEKEZAJI, ataanza kukuuliza kwani wewe una fedha za kutosha. Wengi wamekuwa wanaamini kwamba ili uwe MWEKEZAJI unapaswa kuwa na mamilioni na mamilioni, ila ukiwa kiasi kidogo tu basi hufai kuwa MWEKEZAJI.

Siku siyo nyingi mtandaoni kulikuwa na kichekesho kilichowagawa watu kwenye vipengele kulingana na ukubwa wa kipato chao.

Kilikuwa kinasema hivi

Kama wewe

una maelfu ya fedha basi wewe ni elfunea

Una malaki ya fedha basi wewe ni lakionea

Una mamilioni ya fedha basi wewe ni milionea

Una mabilioni ya fedha basi wewe ni bilionea.

Una matrilioni ya fedha basi wewe ni trilionea

Una mazilioni ya fedha basi wewe ni zilionea.

Tujuane wewe uko wapi?

Japo kililenga kuchekesha watu Ila kwetu kina funzo kubwa sana. Na funzo hili ni kwamba kulingana na imani ya watu wengi kuhusu UWEKEZAJI kama wewe ni elfunea au lakionea basi huwezi kuwa MWEKEZAJI.

Hata hivyo tunaenda kuona muda sio mrefu kuwa huhitaji kuwa milionea au bilionea ili uwekeze, unaweza kuanza KUWEKEZA kutokea popote  ulipo.


2 responses to “UWEKEZAJI NI NINI?”

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X