Wateja wako wasikusahau


Hakikisha kila mara unawasiliana na wateja wako. Usipowasiliana na wateja wako mara kwa mara watakusahau na hata kushindwa kuja kununua kwako. Kitu hiki kinaweza kupekelekea wateja wako kwenda kununua kwa washindani wako.

Weka utaratibu wa kuwasiliana na wateja wako kila mara.

Tafuta sababu (excuse) nzuri ya kuwasiliana na wateja wako.
Mfano siku ya kuzaliwa kwao wapigie simu au watumie ujumbe.
Siku ya kuzaliwa kwa ndugu yake mpigie simu.
Watakie kheri ya mwezi mwezi mpya.
Watakie kheri ya sikukuu yoyote.

Katika kuongea nao kihivyo, utakuta kwamba unaweza kufanya mauzo na hao wateja wako.

Tumia kifurushi chako cha kila mara. Kuongea na wateja wako.

Kila la kheri
Umekuwa nami
Godius Rweyongeza
0755848391
Morogoro-Tz
Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X