Zama Zimebadilika (Part 1)


UTANGULIZI

Dunia tunamoishi sasa imepitia katika nyakati mbali mbali kwa vipindi mbali mbali. Dunia hii imekumbana na vitu mbali mbali ambavyo vimekuwa vikiiweka hii katika vipindi kadha wa kadha ambavyo tunaviita zama. Zama ni nini? Kamusi ya Kiswahili sanifu inazizungumzia zama kama nyakati. Kwa hiyo tungeweza kusema kwamba nyakati sasa zimebadilika badala ya kusema kwamba zama zimebadilika..

Kwa nini tunasema kwamba zama zimebadilika?

Zama ni kipindi ambacho matumizi ya kitu fulani yanakuwa juu sana na ndio  yanakuwa yanatawala kwa hali ya juu. Ukiilewa dhana hii tu utaelewa mengi kutoka kwenye kitabu hiki. Dunia yetu imepitia katika vipindi hivi vingi, kuanzia hapo wanadamu walipoanza kuishi kwenye hii dunia mpaka leo. Kila kipindi kimekuwa na kitu fulani ambacho kinaifanya kipindi kile kiwe chenye utofauti mkubwa sana. Mwanzo kabisa dunia ilipitia katika zama za mawe, baadae ikaja kwenye zama za chuma na baada ya hapo ikaja kwenye zama za viwanda lakini pia ikatoka kwenye zama za viwanda na kuhamia katika zama nyingine ambazo ndizo tulizopo sasa hivi. Na zama hizi ambazo tulizopo sasa hivi hazitaendelea kudumu kwa kipindi kirefu sana maana zitabadilika na kutakuwa na ujio wa zama nyingine.

Kwa hiyo, ni muhimu sana kujua kwamba zama za sasa hivi zimebadilika, tena sana. kuwa na taarifa kwamba zama za sasa hivi zimebadilika ni hatua moja kwenda katika mafanikio. Maana kama hata hauna taarifa kwaba zama za sasa hivi zimebadililka basi ni hatua moja kurudi nyuma.

Kwenye kila zama huwa kuna zana fulani ambayo ndiyo huwa ni msingi mkuu wa uzalishaji. Ndio maana tangu mwanzo nimekwambia ukiilewa maana ya zama, utaelewa mengi kutoka kwenye kitabu hiki.

Kwa kukumbusha tu ni kwamba “zama ni kipindi ambacho matumizi ya kitu fulani yanakuwa juu sana”.

Kwenye zama z mawe. Jiwe ndilo lilikuwa msingi mkuu na lilikuwa linahitajika sana. kwa hiyo kwenye hiyo zama, watoto waliozaliwa na kukua walielekezwa namna ya kutafuta mawe mazuri kwa ajili ya kuwinda, kutafuta mizizi, kujilinda dhidi ya maadui, na hata mapango mazuri ya kuishi. Hizo ndizo zilikuwa zama za mawe. Ulichokuwa unahitaji kwenye hii dunia ilikuwa ni kuwa na jiwe sahihi kwa wakati sahihi ili uweze kutoboa maisha.

Baadaye zama za mawe ziliisha na zama za chuma zikawa zimeingia. Kwenye zama hizi, kitu kikubwa ambacho kilikuwa kinahitajika kwenye hizi zama ilikuwa ni chuma. Aliyekuwa na chuma kwa wakati husika ndiye alikuwa mshindi. Chuma ndicho kilitumika kutafuta chakula, kuwinda, kujilinda na kujikinga dhidi ya maadui.

Hivyo, watoto waliozaliwa na kukulia kwenye hiki kipindi walipewa ushauri nakuaminishwa kwamba ili utoboe kwenye maisha unapaswa kuwa na chuma. Na huo ndio ulikuwa ukweli.

Baada ya zama za chuma yalifuata mapinduzi ya viwanda. Hiki nacho kilikuwa  ni kipindi muhimu sana, kwenye zama hizi hapa kiwanda ndiyo ulikuwa msingi mkuu wa uzalishaji na mtu yeyote ambaye alikuwa na kiwanda alikuwa na uwezo wa kufanya vizuri na kutoboa kimaisha. Zama za viwanda zilizalisha makundi mawili ya watu.

Kundi la kwanza ni la wamiliki wa viwanda. Na kundi la pili ni la waajiriwa kwenye viwanda. Kwa mara ya kwanza watu walianza kuajiriwa na kupewa ujira kwenye zama hizi. Kundi la pili ndilo lilikuwa na watu wengi kulinganisha na kundi la kwanza.

Hivyo, watoto waliozaliwa kwenye kipindi hiki walielewa vitu viwili. Kwanza ni kwamba ili ufanikiwe ni lazima uwe na kiwanda na pili ni kuwa ili ufanikiwe  unapaswa kuajiriwa kwenye kiwanda. Na huo ndio ulikuwa mwanzo wa usemi maarufu wa soma kwa bidii, ili uje ujiriwe kwenye kampuni itakayokulipa vizuri.

Pata ebook hii yote kwa elfu 3 tu


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X