Jinsi Mafanikio Makubwa Yanavyojengwa


Picha hapo chini ni picha ya jengo la Taj Mahal. Jengo hili lipo kwenye Maajabu Saba ya dunia.
Hili jengo lilichukua miaka 22 kujengwa Mpaka kukamilika.

Jengo la Taj Mahal

Hiki kitu kikupe picha ya kuwa vitu vizuri kwenye maisha huwa haviji kirahisj. Najua unapenda sana kupata vitu vizuri, lakini vitu vizuri huwa haviji kirahisi. Ni mchakato.

Ndio maana wahenga wetu wanasema kwamba hata mbuyu ulianza kama mchicha. Hii ni kuonesha kuwa vitu vizuri, vipo, lakini vinajengeka kidogokidogo.

Tena wakati mwingine vinaweza kuonekama vinaanza kimasihala vile.

Ebu fikiria kama wajenzi wa ghorofa. Ukikuta wanaanza kujenga ghorofa, wewe mwenyewe unaweza kufikiri wamechanganyikiwa. Eti wanajenga ghorofa Ila wanaanza kwa kushuka chini. Hahaha
Wanachimba shimo reeefu kwenda chini…

Hivi ndivyo mazuri yanavyoanza, siyo kwamba mara zote mazuri yataanza kwa uzuri wake. Muda mwingine msingi unajengwa kwanza, halafu ndio Mambo mengine yanafuata.

Rafiki yangu, labda nisisitize tu. Ni kitu gani unapenda kufikia au kupata maishani mwako?

Basi kipe muda. Anza kukifanyia kazi taratibu bila kuchoka. Kumbuka kwamba inawezekana kama hautarudi nyuma.

Hatua moja moja itakufikisha mbali tu.

Inawezekana. Kila la KHERI
Godius Rweyongeza
0755848391
Morogoro-Tz

NB: Kama umependa makala hii utapenda pia mafunzo ninayotuma kwa baruapepe. Jaza taarifa zako hapa chini ili uwe miongoni mwa watu wanaopokea mafunzo haya


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X