Abraham Lincoln aliwahi kunukuliwa akisema kuwa, rafiki yangu wa kweli ni yule ambaye atanipa kitabu.
Nadhani huu usemi una maana kubwa katika ulimwengu wa leo kuliko hata alipousema.
Ebu fikiria katika ulimwengu wa sasa ambapo kila mtu anapenda kupewa simu mpya na ya kisasa kama zawadi.
Ulimwegu ambapo watu wanapenda kupewa zawadi ambazo ukifungua utaonekana kwa nje kuwa wewe ni wa viwango!
Je, ukipewa zawadi ya kitabu si ina maana kubwa zaidi?
Kwa kulitambua hilo, nimeona ni vyema kabisa na wewe nikupe zawadi ya kitabu changu pendwa cha Kiswahili. Kipate hapa