Kiwango Cha Elimu Unachopaswa Kuwa nacho ili uandike kitabu


Leo nimepokea ujumbe wa MTU anateniuliza, kiwango gani Cha Elimu unapaswa kuwa nacho ili uandike kitabu?

Swali hili limenivutia sana kiasi kwamba nimeona niandike Makala na kuileta kwako.

Kwenye ulimwengu wa uandishi kuna waandishi wa kila aina.

Kuna waandishi wenye PHD,
Kuna waandishi wenye shahada moja
Kuna waandishi ambao wameishia darasa la saba n.k.

Kwa hiyo, hakuna kiwango maalumu cha elimu ambacho MTU anatakiwa kuwa nacho.

Kitu kikubwa kwenye uandishi ni mwandishi kuhakikisha ameijua mada anayoiandikia kiundani. Ameitafiti na kuifuatilia nje ndani.

Hicho ndiyo kitu muhimu sana.

Kiufupi ni kwamba kama unajua kusoma na kuandika Basi unapaswa kuandika.


One response to “Kiwango Cha Elimu Unachopaswa Kuwa nacho ili uandike kitabu”

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X