Kwa Nini Unasherehekea Mabadiliko Yaliyo Nje Ya Uwezo Wako Pekee?


Kuna watu vitu ambavyo huwa wanasherehekea kama mafanikio yao ni vile vitu vilivyo nje ya uwezo wao. Yaani, watu wanasherehekea sherehe kama pasaka, idi, siku za kuzaliwa,…

Haya yote ni mabadiliko ambayo yanatokea kila mwaka, ila mabadiliko haya yapo nje ya uwezo wako. Wewe siyo unayesabisha mabadiliko haya, badala yake kalenda iko hivyo. Kwa mfano, wewe huwezi kuamua kwamba mwaka huu sikukuu ya uhuru isherehekewe siku nyingine tofauti na ile iliyozoeleka. Hata hivyo, kuna mabadiliko ambayo unaweza kufanya kwenye maisha yako. Na mabadiliko haya yanaweza kuleta utofauti.

Kuanzia mwaka huu unapaswa sasa kuamua kwamba wewe huendi kusherehekea mabadiliko ambayo ni ya kalenda tu. badaa yake unaenda kufanya mambo ya tofauti yatakayokupelekea wewe kupata matokeo ya tofauti. Na hivyo, kukuwezesha kusherehekea mafanikio yaliyotokana na juhudi zako pia


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X