Nilipokuwa mdogo, nilikuwa napenda sana kusikiliza redio. Kila siku SAA kumi na mbili asubuhi ilikuwa lazima nisikilize DW habari za ulimwengu. Mchana na jioni ilikuwa hivyo hivyo, yaani, ilikuwa kama dozi .
Siku moja wakati nasikiliza habari, walitangaza kwamba kufikia mwaka 2050 kuna viumbe watakuwa wamepotea na kutoweka kwenye uso wa dunia.
Watu niliokuwa nao walianza kulalamika. Kila mtu alishangaa kuona ni kwa nini wanazungumzia mambo ya mwaka 2050 sasa. Wakati bado kuna muda mwingi sana. Rafiki yangu mmoja alithubutu kusema ni uongo. Huku mwingine akisema wazungu wanapoteza sana muda.
Hali hii inaweza kukupa picha ni kwa jinsi gani watu hawataki kuangalia mbeleni. Ni kwa jinsi gani watu hawana mipango ya mbeleni.
Labda nikuulize wewe unataka uwe umefikia Nini mpaka mwaka 2050?
Najua..
Najua..
Najua utaniambia umri wangu umeenda kwa hiyo 2050 ni mbali. Sawa, na mimi nakubaliana na wewe.
Ila vipi una mpango wa hata wa miaka 10 au mitano? Au na penyewe ni mbali?
Andika Malengo yako ya miaka 1/2/3/5/10/25.
Watu wengi wanaamini katika msemo unaosema leo ni leo asemaye kesho ni mwongo. Hali hii imewafanya watu wengi kusitasita kuweka mipango yao ya muda mrefu. Hivyo kuamini kwamba kila wanachopata sasa ni kwa ajili ya sasa na kesho itajipa yenyewe. Hali hii itakunyima motisha ya kusonga mbele na kufanya mambo makubwa.
Mara zote na siku zote unapaswa kuwa na mpango na ndoto za muda mrefu.
Unapaswa kupanga kama vile utaishi milele na kufanyia mipango yako leo kama vile utakufa kesho.
Siku siyo nyingi nilikuwa nasoma wasifu wa Jack Ma. Unaitwa Alibaba: The House That Jack Ma Built.
Ndani yake mwandishi anasema kwamba wakati Jack Ma anaanzisha kampuni ya ALIBABA alikuwa na mpango wa kufanya kampuni hiyo idumu kwa miaka 102.
Miaka 102 ni mingi, wachache sana wanaishi hiyo miaka.
Ila jamaa alianzisha kampuni yake na huo mpango.
Kampuni ya Alibaba ilianzishwa mwaka 1999 na Jack Ma alikuwa tayari na miaka 36. Maana yake tunapozungumzia miaka 102 baada ya hiyo kampuni kuanzishwa, tunaiongelea miaka ya 2101!!!!!!
Sidhani kama Jack Ma atakuwa bado anaishi, Ila huyu jamaa ana maono makubwa ya kufikiri mpaka huko atakapokuwa ameshaaga dunia ..
Hii ndio nguvu ya maono, MTU mwenye maono ya mpaka mwaka 2101. Siyo sawa na mtu mwenye lengo la kulala leo na kuamka kesho akaonane na mchepuko wake!
Na wewe kuanzia Leo weka maono ya muda mrefu. Unaweza usiwe hai hiyo miaka. Lakini maono yako hayatakufa. Ndio maana tunapaswa kufanya vitu kwa kuwafirikia hata wanetu…ili waweze kuwa waendelezaji wa vitu tulivyoanzisha. Tunaoneahe runavyofanya ili na waweze kuwa waendelezaji wa kile tunachofanya…
NB. Kama bado hujapata nakala ya kitabu cha KUTOKA SIFURI MPAKA KILELENI, fanya hivyo leo. Nakala ngumu ni 20,000
Nakala laini ni 10,000 tu.
3 responses to “Mipango yangu ya miaka 100 ijayo”
Napenda sana makala zako Kiongozi
Karibu sana ndugu yangu. Tuko pamoja
Napenda sana maandiko yako