[eBOOK MPYA] NGUVU YA KUTOA (THE MAGIC OF GIVING)


Utangulizi

Rafiki yangu kuna nguvu kubwa sana katika kutoa. Hii ni tabia ambayo unapaswa kujifunza na kuifanyia kazi kila siku. Nadhani utakuwa umewahi kusikia kuwa matajiri wana hadi mashirika ambayo yanahusika na utoaji. Kwa mfano, Bill Gates ana shirika la GATES AND MELINDA FOUNDATION. Elon Musk ana shirika la MUSK FOUNDATION na mabilionea wengine pia wana mashirika au tasisi zinahousika na utoaji au la wamejiunga moja kwa moja na shirika la Bill Gates au shirika jingine ambalo wao wameona linawafaa. Hii ni kwa sababu kutoa kuna nguvu kubwa sana kwenye maisha.

Kwa asili ni kwamba, kadiri unavyotoa ndivyo unapokea zaidi. haupungukiwi chochote kile unapotoa. Ndio maana unaona kwamba mabilionea wanaotoa, wanazidi kuwa mabilionea zaidi na zaidi. Kutoa kwao hakuwafanyi washindwe kuendelea kukua zaidi. kwa hiyo kama ulikuwa unaamini kuwa ukitoa labda utaishiwa, siyo kweli.

Hivyo na wewe anza kujenga utaratibu wa kutoa. Hakikisha kwamba kwako haipiti siku bila ya wewe kuwa umetoa kitu chochote kile hata kama kitu hicho ni kidogo. unaweza kununua hata mfuko wa pipi na kila siku ukawa unatoa pipi moja tu kwa mtu mmoja kwa mwezi mzima. Na siyo kwamba utoe kwa mtu huyo huyo huyo kila siku. Bali kila siku toa kwa mtu yeyote kitu. Hii itaimarisha misuli yako ya kutoa. Mwanzoni unapoanza utaratibu wa kutoa kwa watu, kinakuwa ni kitu kigumu lakini kadiri unavyoendelea misuli yako inazidi kuimarika na hivyo unajikuta kwamba unaweza kutoa vizuri tu bila shida yoyote.

Sasa hili suala la kutoa linaweza kuwa linakuchanganya kidogo. wewe unaweza kuwa unaona kwamba hauna kitu cha kutoa. Au pengine unasubiri mpaka pale utakapokuwa milionea au bilionea ili utoea. Ila ukweli ni kwamba hakuna binadamu ambaye ni masikini kiasi cha kukosa kitu cha kutoa. Hivyo, katika ngazi yoyote ile ulipo, una uwezo wa KUTOA

Ninatoa nini sasa wakati sina fedha?

Na hapa ninapozungumzia kutoa simaanishi kwamba, utoe fedha peke yake. Fedha ni kipengele kimojawapo cha kutoa kwa watu. Ila kuna vitu vingine ambavyo unaweza kutoa ikiwa ni pamoja na muda wako, nguvu zako, furaha yako, kuwasaidia watu kutengeneza maisha bora na utajiri, kuwaburudisha watu kwa kipaji chako, kuwashirikisha wengine maarifa, makala na vitabu n.k


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X