1.Siri ya kuwa Kiongozi Bora kuwasikiliza watu wako na kuwa karibu na watu wako.
Mwandishi anasema kwamba hiki Ni kitu ambacho alijifunza kutoka kwa babu yake na alikuja kukifanyia kazi yeye mwenyewe kwenye maisha yake.
Ukiwa karibu na watu wako ni rahisi kujua matatizo yao na hivyo kujua wanataka Nini?
2. Unapaswa kubadilika la sivyo mabadiliko yatakubadilisha. Huu ni usemi ambao aliusema kwenye hotuba yake mwaka 2004 wakati akihutubia viongozi wa nchi za kiarabu.
Miaka 60 na 70 nchi nyingi za kiarabu zilifanya mapinduzi ya kivita. Na wote waliokuwa wanafanya mapinduzi kuna aina fulani ya maisha walikuwa wanataka. Wengi walikuwa wanaona viongozi hawatendi haki na wananchi wanaonewa. Lakini baada ya wao kuingia madarakani walisahau hilo na kuanza kufanya yaleyale ambayo wao walikuwa hawataki.
Na hapo ndipo aliwaambia kuwa BADILIKA au la sivyo mtabadilishwa.
Hapa Kuna somo kubwa sana kwetu. Watu wengi huwa wanapenda kuhubiri mabadiliko Ila wao wenyewe huwa hawapo tayari kubadilika.
Ngoja nikwambie kama unataka mabadiliko, basi anza wewe kubadilika la sivyo utabadilishwa.
Kama ungependa kupata kitabu hiki jaza taarifa zako hapa chini, nitakutumia kwako bila kuchelewa
Kila la kheri
Umekuwa nami
Godius Rweyongeza
0755848391
Morogoro-Tz
2 responses to “Siri Mbili Za kuwa Kiongozi Bora Kutoka Kwenye Kitabu Cha My Story Cha Sheikh Mohammed bin Rashid Al Maktoum”
Thanks
Well