UAMINIFU NI MTAJI


Mwaka 2018, nilisafiri kwenda Arusha na baadaye nikaenda Bukoba kwa wazee kusalimia. Ilikuwa ni safari ya zaidi ya mwezi…

Nikiwa Arusha kuna jamaa alinitafuta. Alikuwa mshikaji ninayemfahamu. Au basi niseme tulikuwa tunasoma wote pale SUA.

Aliniambia anataka nimkope fedha kama laki tano hivi, na angenirudishia hiyo fedha ndani ya wiki…
Kuna fedha alikuwa anaisikilizia….

Nilimwambia wiki moja siyo kubwa sana, subiri wiki ipite, utapata hiyo fedha unayoisikilizia na utaendelea na kazi zako.

Alivyo niganda sana, nikamwambia nipo safarini (of course na mwenyewe alikuwa anajua hili) na nimewacha mtu kwenye biashara yangu. Fedha isingeweza kutolewa bila ya mimi kuwepo kuweka sahihi (kitu ambacho kilikuwa kweli pia).

Akatulia…

Sasa ngoja nifupishe stori. Mwaka mmoja baadaye nilikuja kupata taarifa kuwa kumbe kipindi kile anakopa kwangu, alikuwa akikopa kwa wengine pia.

Kuna ambao tulikuwa wagumu na hatukutoa fedha zetu na wengine walimpa. Kitu ambacho siyo kibaya…

Ila sasa huyu jamaa hakuwarudishia fedha zao….kitu ambacho ni kibaya.

Sasa ninachotaka niseme leo ni nini?

Kwanza, nataka niseme kwamba uaminifu ni mtaji. Ukiaminiwa aminika.

Pili, nataka niseme kwamba, upende hela zako. Hakuna mtu mwingine anayeweza kupenda fedha zako kama wewe. Hakuna.

Tatu, usipende kukopa kama hauedeshi microfinance ya kukopesha. Si unajua kukopa harusi….au umesahau..

Nne, jiongezee kipato chako katika namna ambayo hutahitaji kukopa tena maishani mwako.

Ni hayo tu.

Mpaka wakati mwingine
Mimi ni Godius Rweyongeza

Hakikisha umejiunga na mfumo wetu wa kupata mafunzo zaidi kwa kujaza taarifa zako hapa chini.👇🏿👇🏿


3 responses to “UAMINIFU NI MTAJI”

  1. Uaminifu ni kila kitu.
    Wengi wanaofanikiwa na kufika mbali uaminifu umekuwa na mchango mkubwa sana.
    Kila mtu anapenda kufanya kazi na watu waaminifu.

    Barikiwa sana Mr Godius

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X