Wazo Bora La Biashara


Najua kila mtu anapenda kupata wazo zuri la biashara. Ukweli ni kwamba WAZO ZURI LA BIASHARA NI LILE AMBALO UNAWEZA KUFANYIA KAZI KWA SIKU 365 BILA KUCHOKA. Usipolifanyia kazi wazo lako, ujue utalinyima uhai.

Ebu fikiria mtu ana wazo la kuchonga sanamu fulani, halafu hilo wazo akakaa nalo kichwani mwake.

Unadhani wewe utaiona hiyo sanamu? Jibu ni hapana, kwa sababu sanamu hiyo haijachongwa. Kuchonga sanamu ni kuipa uhai, na hivyo kuifanya ionekane kwa watu wengine. Raha ya wazo sharti ulifanyie kazi na kufanyia kazi wazo lako.

unafanya wazo liwe bora.

Najua kitu hiki kinaweza kukushangaza kutokana na ukweli kuwa umeaminishwa kuwa wazo zuri la biashara ni lile ambalo linalipa. Labda nikuulize kuwa unajuaje wazo linalolipa na ambalo halilipi? Kwa hapa unaweza kujitetea na kusema wazo la kuanzisha mtandao kama Google, Facebook, au wazo la kutengeneza simu janja ni wazo ambalo lilikuwa linalipa pia. Ukweli ni kuwa mawazo haya yote yalikuwa hayana maana yoyote. Ni mpaka pale yalipofanyiwa kazi.

Steve Jobs aliifanyia kazi iPhone kwa zaidi ya miaka miwili na nusu kabla haijaonekana kwenye uhalisia. Wazo la kuanzisha facebook halikuwa hata wazo bora, ni mpaka pale lilipofanyiwa kazi.

Wazo la kuanzisha kampuni ya cocacola pia siyo kwamba lilikuwa ni wazo bora, ni mpaka pale lilipofanyiwa kazi. Sasa wewe kama huwezi kufanyia kazi wazo lako kwa siku 365 zijazo tu.

Linaweza lisije kuleta manufaa yoyote maishani. Utaaishia kufa nalo na kwenda kujaza makaburi na wazo lako zuri. Kitu kikubwa cha kuondoka nacho kwenye kipengele hiki ni kwamba unapaswa kuanza kufanyia kazi wazo lako, tena unapaswa kuanza kulifanyia kazi leo hii. Kila la kheri


One response to “Wazo Bora La Biashara”

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X