Rafiki yangu, unapofanya kitu kikaenda ndivyo sivyo, usikate tamaa.
Kwa sababu kadiri unavyokosea ndivyo unazidi kuwa imara zaidi.
Makosa ni mwalimu mzuri kama utayatumia vizuri. Ndio maana wahenga wetu wanasema kufanya kosa siyo kosa. Kosa ni kurudia kosa.
Ukirudia kosa maana yake hukukifunza chochote na wala hukupata funzo lolote kutokana na kosa la kwanza.
Na ukiendele kurudia kosa lilelile kila Mara, huwezi kupiga hatua kubwa kimaisha.
Sasa labda nikuulize wewe makosa ambayo huwa yanatokea kila siku kwenye maisha yako, huwa yanakuimarisha au huwa yanakubomoa?