Fanya Yafuatayo Kuepuka Kuwa Miongoni mwa Walalamikaji


Moja ya kitu rahisi sana ni kulalamika. Kila mtu anaweza kukifanya. Lakini kitu kigumu kufanya ni vitendo na kuonesha matokeo.

Sasa siku ya leo, nataka uepukane na malalamishi ili mwisho wa siku uwe mtu wa kuleta matokeo ambayo wewe mwenyewe unayatamani

Unajua kwa Nini Watu wanalalamika?

Kwa sababu kuna matokeo mazuri wanayataka ila  wanataka mtu mwingine awasaidie kupata hayo matokeo. Kwa hiyo, wanataka MTU mwingine azalishe matokeo na siyo wao.

Mtu anataka kupata afya njema, anawalaumu wazungu kwa kuleta vyakula vya makopo.

Mtu anataka utajiri na fedha, anailaumu serikali kwa kutokutoa hela. Wakati fedha chanzo chake ni thamani.

Sasa badala ya kulaumu, sikiliza. Kuwa mtu wa kuzalisha matokeo.

Kwanza, kuwa na malengo ambayo unayafanyia kazi. Zama kwenye kufanyia kazi malengo yako na sahau Mambo mengine

Pili, kabla ya kulaumu jiulize wewe umezalisha matokeo gani. Kila utakapojiuliza swali hili, utakuta kwamba unalazimika kukazana na malengo yako zaidi kuliko kulaumu MTU mwingine

Tatu, fahamu kuwa maisha ni wajibu wako. Hakuna mtu mwingine ambaye anaweza kupiga push-up kwa ajili yako.

Nne, usifuatilie maisha ya watu wengine. Kadiri unavyofuatilia maisha ya watu wengine, ndivyo unavyojinyima fursa ya kufanyia kazi malengo yako.

Tano, Mara zote kuwa mtu wa kujifunza na kusoma vitabu. Jifunze , jifunze jifunze.

Kila la kheri.

Umekuwa nami
Godius Rweyongeza kutoka SONGAMBELE CONSULTANCY
0755848391
Morogoro-Tz


2 responses to “Fanya Yafuatayo Kuepuka Kuwa Miongoni mwa Walalamikaji”

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X