Wachezaji Lionel Messi na Ronaldo wanacheza dakika 90 uwanjani na wanalipwa kiasi kikubwa Cha fedha kuliko wachezaji wengine.
Unadhani kwa nini wanalipwaa kiasi kikubwa hivyo? Ni kwa sababu ya thamani yao wanayotoa.
Kitu chenye thamani kubwa kinauzwa kwa bei kubwa ukilinganisha na kitu chenye thamani ya ndogo.
Kama unataka kupata fedha basi unapaswa kuwa tayari kutoa thamani kwa watu.
Labda unajiuliza, thamani ni kitu gani? Na Mimi nawezaje kuongeza thamani kwa watu.
Iko hivi, ebu chukulia sasa hivi umetoka nje na umekutana na sura ngeni mtaani kwako. Mgeni akakuuliza, naomba kujua kwa mzee Daudi. Na wewe Daudi unamjua ni mzee pale nyumba ya tatu kutoka UNAPOKAA.. ukasema ngoja nimpeleke huyu jamaa mpaka kwa mzee Daudi…
Kwa upande wako unakuwa umetoa thamani…
Huyu jamaa alikuwa na shida na na umemwonesha kwa mzee Daudi, na shida yake imeisha.
Tungekuwa sehemu nyingine, basi ilibidi akulipe jero kwa kitendo cha kukuuliza kwa mzee Daudi ni wapi na buku ya kumwonesha kwa mzee Daudi….Hahah
Ulivyomfikisha yule jamaa kwa mzee Daudi amefurahi, kuthibitishwa kwamba amepata thamani kutoka kwako.
Hivyohivyo kwa fedha, fedha ni matokeo ya thamani unayotoa..
Unataka watu wakulipe? Toa thamani..
Ukitatua matatizo ya watu, unakuwa umetoa thamani.
Ukisogeza huduma karibu yao, unakuwa umeongeza thamani.
Kwa hiyo badala ya kukazana kuikimbiza fedha, kazana kutoa thamani kwanza. Fedha itakuja tu.
Sijui umenielewa….
Kama umenielewa kaangalie video hii YouTube kwanza, Kisha SUBSCRIBE
anyaway, tuendelee..
Si umewahi kusikia habari za fuata nyuki ule asali. Unajua kwa Nini Watu wanawafuafa nyuki mbali na kuwa nyuki ni wakali..
Kwa sababu nyuki wanatoa thamani kubwa kiasi hakuna MTU anayeweza kuitega mgongo.
ukizalisha thamani nzuri watu watakuwa tayari kukufuata hata Kama upo kijijini. Kwani nyuki huwa tunawafuata wapi?
Hakuna nyuki wenye mzinga Kariakoo… Mizinga yote ipo misituni Ila tunawafuata tu. Rafiki yangu, zalisha thamani…
Bado tuko pamoja? Basi mpaka hapa Sina shaka utapendaa kitabu changu cha KUTOKA SIFURI MPAKA KILELENI. Kitabu hiki Ni 20,000 tu na unatumiwa popote ulipo duniani.
wasiliana na 0755848391 kukipata.
Umekuwa nami
Godius Rweyongeza kutoka SONGAMBELE CONSULTANCY
0755848391
Morogoro-Tz
One response to “Fedha Chanzo Chake Ni Thamani”
Thanks 😁 it’s great