Hii Ndio Aina Bora Uwekezaji Unayoweza Kufanya. Hakuna Uwekezaji Wenye Manufaa Kama Huu


Moja ya kitu ambacho watu wanatafuta na wangependa kupata maishani mwao ni uwekezaji mzuri. Najua na wewe unasoma hapa kwa sababu unataka uwekeze fedha zako sehemu ambayo itakupa faida kubwa. Sasa siku ya leo nataka nikwambie eneo zuri ambalo wewe mwenyewe unaweza kuwekeza na kupata faida.

Kwa siku sasa nimekuwa nikikwambia maeneo ya kuwekeza na hasa kwenye hisa, hatifungani na VIPANDE.

Huu Ni uwekezaji mzuri ambao hado nashauri uufanye, Tena kwa nguvu zako zote.

Ikiwezekana tumia nguvu ya vitu vidogo kufanya uwekezaji huu. Yaani, anza kuwekeza kidogo kidogo, Kisha endelea kuwekeza kidogo kidogo bila kuacha kwa muda mrefu. Hiki kitu kidogo unachowekeza baada ya muda mrefu kitageuka kuwa kikubwa kwa kutumia kanuni ya riba mkusanyiko.

Ila ukiachana na huu uwekezaji wa Hisa, hatifungani na vipande kuna uwekezaji mwingine mzuri ambao unaweza kuufanya na ukakupa faida kubwa pia. Na uwekezaji huu ni Kuwekeza kwenye matangazo ya BIASHARA yako.

Huu ni uwekezaji mwingine ambao unaweza kuufanya, ukakupa faida na matokeo kwa muda mrefu ujao.

Matangazo mara zote yanalenga kuleta wateja watakaonunua bidhaa fulani kwenye BIASHARA yako. Sasa matangazo yako yakifanyika vizuri, yana uwezo wa kuleta matokeo makubwa kuliko uwekezaji mwingine ambao tayari nimekwambia hapo mwanzoni.

Kwa Nini?
Kwa sababu, takwimu zinaoneshwa kuwa WAWEKEZAJI wakubwa kwenye soko la hisa, hatifungani, vipande na hata WAWEKEZAJI wa  fedha za kigeni huwa wanapata faida yenye ukomo.
Mwekezaji Warren Buffet ndiye mwekezaji mwenye mafanikio ambaye huongelewa sana linapokuja suala zima la uwekezaji. Ila takwimu zinaoneshwa kuwa huwa anapata faida ya asilimia 20% ukuaji wa mwaka.

Siyo Warren Buffet peke yake tu, hata WAWEKEZAJI wengine kama
Carl Icahn anapata  31% ya ukuaji kwa mwaka.
George Soros anapata 20% ukuaji wa mwaka.
Peter Lynch anapata 29% ya ukuaji wa mwaka.

Kwa hiyo nataka kusema tusiwekeze?
Hapana. Ninapenda uwekezaji na Mara zote nimekuwa nikishauri uwekeze kwenye HISA, hatifungani na vipande. Kama Bado hujafungua akaunti yako ya uwekezaji, ujue wazo kuwa unajinyima fursa nzuri ya kupata faida kwa muda mrefu. Kafungue akaunti Leo hii na uanze kuweka fedha kidogo kidogo kama uwekezaji. Nimeandika mpaka kitabu cha uwekezaji kwenye hisa. Kinaitwa MAAJABU YA KUWEKEZA KWENYE HISA, HATIFUNGANI NA VIPANDE.

Ila sasa kikubwa ninachotaka ufanye pia ni Kuwekeza kwenye matangazo ya BIASHARA yako . Itangaze BIASHARA yako Mara kwa Mara na kila sehemu ambayo unajua inaweza kukuletea wateja. Huu ni uwekezaji ambao una faida kubwa sana.

Ukifanya tangazo lako vizuri, utakuta kuwa tangazo Hilo linakuletea faida kubwa hata Mara 10 ya ule uwekezaji uliofanya mwanzoni.

Unaweza kuwekeza laki moja ukapata mpaka faida ya milioni. Yaani, unatangaza kwa laki moja, unapata faida ya milioni moja. Faida ambayo ni ngumu kuipata kwenye uwekezaji wa kawaida wa hisa, hatifungani na vipande.

Hivyo kumbe, BIASHARA yako inapaswa kuwa sehemu ya kwanza kabisa ambapo utafanya uwekezaji. Kisha baada ya hapo wekeza maeneo mengine.

Je, upo tayari kuwekeza kwenye BIASHARA yako na kuikuza kwa viwango vikubwa? Upo tayari?
Kama upo tayari kuikuza BIASHARA yako kwa viwango vikubwa, nashauri usome kitabu changu cha NGUVU YA VITU VIDOGO KUELEKEA MAFANIKIO MAKUBWA.

Ili uone hii nguvu inavyoweza kufanya kazi kwa ajili yako pia.

Kila la kheri

Umekuwa nami rafiki yako wa ukweli
Godius Rweyongeza
0755848391
Dar-Tz
Kwa maoni, Ushauri na maswali: godiusrweyongeza1@gmail.com

For booking: songanbele.smb@gmail.com2 responses to “Hii Ndio Aina Bora Uwekezaji Unayoweza Kufanya. Hakuna Uwekezaji Wenye Manufaa Kama Huu”

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X