Unaendeleaje rafiki yangu wa ukweli. bila shaka kila kitu kinaenda vizuri upande wa huko. Siku ya leo ningependa nikujuze kazi mbili ambazo huwezi kumwajiri mtu kuzifanya kwa niaba yako. Na kazi hizi siyo nyingine bali ni
Moja kufikiri. Hiki ni kitu ambacho huwezi kumwajiri mtu ili akifanye kwa niaba yako. Badala yake ni kwamba unapaswa ukifanye wewe mwenyewe bila kujali unapitia hali gani. kufikiri kwa ajili ya kesho yako, ni jukumu lako na hakuna mtu ambaye anaweza kufanya hilo kwa niaba yako.
Kufikiri kwa ajili ya kesho ya kampuni au biashara yako, ni jukumu lako na hakuna mtu mwingine ambaye anaweza kufanya hicho kitu kwa niaba yako.
Kwa hiyo kuanzia leo hii, fahamu kuwa huu ni wajibu wako, na hakikisha kwamba unaufanyia kazi..
Pili ni kupanga ratiba yako. Hili ni jukumu lako jingine ambalo huwezi kumwajiri mtu kulifanya kwa niaba yako. Wewe mwenyewe unapaswa kuwa tayari kulifanya. Kila mwishoni mwa wiki unapaswa kutenga muda maalumu ambapo utaipangilia wiki yako. Muda ambapo utafanya na kukamilisha majukumu ya wiki ijayo. Na kila siku jioni unapaswa kupanga ratiba ya kesho yako. Kiasi kwamba ukiamka tu asubuhi, basi unaanza kuifanyia kazi hiyo ratiba kama ambavyo umeipangilia.
Sikiliza kitu kimoja, kama huwezi kupangilia ratiba yako kwa ufanisi na ubora unaotakiwa, unapaswa kujua kwamba majukumu yako utayafanya hovyohovyo. Sasa kazi ni kwako. je, upo tayari kufanya majukumu yako hovyohovyo au utaanza kupangilia ratiba yako kiufanisi?
One response to “Hii ni kazi anbayo huwezi kuajiri mtu kuifanya kwa niaba yako”
[…] soma zaidi: Hii ni kazi anbayo huwezi kuajiri mtu kuifanya kwa niaba yako […]