Historia ya Kiswahili 
Ukisoma historia ya Kiswahili  unaona kwamba kilianza kimasihala tu. Kilianza kutumiwa maeneo ya Pwani na baadaye kikasambaa kuja bara na mpaka leo hii, kina wazungumzaji zaidi ya milioni 150. Ni lugha pekee barani afrika ambayo siyo ya kigeni ila watumiaji wengi.
 
Ninataka kusema nini sasa hapa.
Ninataka niseme kwamba, kitu chochote kikubwa huwa hakianzi kwa ukubwa wake.
Mbuyu huwa unaanza kama mchicha.
Wewe pia kwa ndoto yako pia. Usitegemee kwamba ndoto yako kubwa utaifanikisha ndani ya siku moja au wiki. kuwa na ndoto kubwa ila anza kuifanyia kazi kidogo kidogo bila kurudi nyuma.
Juhudi zako kidogo kidogo zinaweza zisionenake ndani ya siku moja, ila baada ya muda hizo juhudi zitakusanyika na kutengeneza kitu kikubwa.
 
Ebu fikiria kwa mfano una ndoto ya kuandika kitabu…
Ukiangalia vitabu vilivyo vingi vina kurasa 200 mpaka 400. Ukifikiria hili tu unakata tamaa. Lakini kabla hili halijakukatisha tamaa, nataka nikwambie kwamba unaweza kuandika kitabu chako kwa kuanza kidogo..
Of course kidogo mwanzoni kitaonekana kama siyo chochote. Utakuwa kama unachota maji kutoka baharini kuweka nchi kavu. Lakini hichohicho kidogo ukikifanya kwa uendelevu, mwisho wa siku kitakuwa kikubwa…
Kwa hiyo, kitabu chako unaanza kukiandika hivi,,
Unakiandika kama unavyoandika ujumbe mfupi…

Kwani wewe kwa siku unaandika jumbe ngapi  au unajibu jumbe ngapi ambazo zinatumwa kwako…
Hivi hizi jumbe unazoandika kila siku baada ya mwaka tukiziunganisha ni sawa na kitabu chenye ukubwa gani? sasa na kitabu chako nataka ukiandike kama unavyoandika ujumbe mfupi…
Badala ya kusubiri ukiandike chote kwa pamoja na kwa siku moja. anza kuandika maneno 100 tu kila siku. Maneno 100 ni sawa na ujumbe mfupi na unaweza kuyaandika ndani ya dakika tatu tu…
Sasa kila siku ukiandika maneno 100 baada ya mwaka ni sawa na maneno 36,500. Hiki tayari ni kitabu kikubwa.

Hivi ndivyo ndoto kubwa zinavyofanyiwa kazi….
Inawezekana wewe ndoto yako siyo kuandika kitabu ila pointi kubwa ninayotaka nikwambie ni kwamba, kwa ndoto yoyote ile uliyonayo basi fikiria namna unavyoweza kuanza kuifanyia kazi leo hii. Na usifanye kazi kwa siku moja kisha ukaacha, endelea kuifanyia kazi kila siku mpaka kieeweke.
Ila kama una ndoto ya kuandika kitabu kweli.. pengine kozi yangu ya uandishi inakuhusu, japo sasa hivi imejaa wanafunzi. Ila wasiliana nami, ntajua namna ya kukupitisha mlango wa nyuma ili ujiunge.
 
Umekuwa nami.
GOdius Rweyongeza kutoka SONGAMBELE
Tuwasiliane kwa 0755848391
Morogoro-Tz
 
 
NB: Ile ofa ya ebooks zangu tatu bado inaendelea kuna watu wanachangamka kujinyakulia hizi ebooks za kipekee, sasa sijui wewe umekwama wapi.

Nashauri sana upate hizi ebooks maana zitakusaidia sana. ebooks zenyewe niNGUVU YA WAZO: Jinsi WAZO LINAVYOWEZA KUBADILI DUNIAKIPAJI NI DHAHABU:  Jinsi ya kugundua, Kunoa na kuendeleza kipaji chakoMITAJI 8 ILIYOKUZUNGUKA NA JINSI YA KUITUMIA.Hizi ebooks ni za kipekee sana, na siyo za kukosa kiukweli. Pata ebooks hizi kwa gaharama ya 12,000 tu leo hii. Utatuma fedha kwa 0755848391 jina ni Godius Rweyongeza. Baada ya hapo utanitumia ujumbe nikutumie hivi vitabu.
Ikumbukwe kwamba hivi vitabu gharama yake ni zaidi ya elfu 30+
 
Baadaye….
 
 
MAKALA YA LEO
 
PODCAST YA LEO


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X