Huu ndio utaratibu mzuri ambao unapaswa kuujenga kuanzia mwezi huu


Moja ya sifa ya watu wanaofanya makubwa kwenye hii dunia ni tabia ya kujifunza. Hii ni tabia moja muhimu ambayo inaweza kukusaidia wewe kufanikisha mambo makubwa kwenye hii dunia. Kama bado unajiuliza ni kwa jinsi gani kusoma kunaweza kukusaidia wewe, chukua hatua. Utoe mwaka mmoja ambapo utajifunza kila siku. Kisha linganisha huo mwaka na miaka mingine ya nyuma ili uweze kuona utofauti.

Baada ya mwaka mmoja, linganisha mwaka wako huo mmoja ambao ulikuwa unasoma vitabu na ile miaka ambayo ulikuwa husomi. Kusoma ni jambo la muhimu sana kwenye maisha yako ya kila siku, kama kula kulivyo muhimu kwenye maisha yako ya kila siku.

Kwa hiyo, anza kujijengea utaratibu wa kusoma vitabu kuanzia leo hii. Lakini, haupaswi kuishia hapo tu. Badala yake unapaswa pia, kujenga utaratibu mzuri wa kununua walau kitabu kimoja kila mwezi. Kila unapopokea mshahara, hakikisha kwamba, unatoa kiasi fulani kwa ajili ya tu ya kununua vitabu au kitabu. Hiki kitu kidogo tu, kinaweza kukusukuma na kukufikisha mbali.

Fedha yako ya kununua kitabu, inaweza kuwa ni fedha hiyohiyo ambayo wewe unatumia kufanya mambo ambayo si ya muhimu kwa sasa.Ila sasa kwa kuwa umejijengea utaratibu huu wa kusoma vitabu. Unaamua kuanza kuiwekeza hii fedha kwa ajli ya baadaye yako.

Rafiki yangu, anzisha huu utaratibu. Nina hakika mwaka mmoja baadaye utanishukuru kwa ajili ya huu utaratibu wa kipekee ambao utakuwa umeuanzisha. Je, upo tayari kwa ajili ya hiki kitu.

Kama upo tayari, anza kuwa kuchukua kitabu cha JINSI YA KUFIKI ANDOTO ZAKO Toleo la 2.

Kwenye hiki kitabu unaenda kujifunza namna ambavyo utaweza kufanikisha ndoto zako kubwa za kimaisha. Je, upo  tayari?


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X