IJUE NJIA YA KUFUATA


Kama haujui njia ambayo unapaswa kuchukua basi njia yoyote ile itkupeleka

Ebu fikiria kitu kama hiki hapa, umeenda stendi ili kukata tiketi, halafu unampa mkata tiketi pesa yako. Na unamwambia kwamba unaomba akupe tiketi unadhani atakuwambiaje? Au au nadhani swali gani atakuuliza? Unaelekwa wapi?  Ebu fikiria unamjibu kwamba sijui. Atakwambia kwamba kama haujui basi rudi nyumbani, kitu kama hiki ndicho huwa kinatokea kwa watu wengi kwenye maisha, yaani huwa kinawatokea watu wengi maishani. Yaani, huwa wanapita kwenye misha bila ya kuwa na mwelekeo. Ni sawa na kwamba huwa wanachukua njia yoyote maishani mwao. Hawajui haswa ni wapi wanaelekea.

Huyu hapaswi kuwa wewe. Hakikisha kwamba unakuwa na ramani ya wapi unaelekea. Jua nini unapaswa kufanya na kw anini unataka kuelekea huko. Jua ni watu gani ambao utapaswa kwenda nao ili uwezeu kufika na gharama ambazo utapaswa kulipa ili kufikia huko. Kama ni fedha jua kiwango cha fedha kitakachohitajika hataka kama ni kwa kukadiria, kisha anza kuweka mkakati wa kuhakikisha kuwa unapata kiasi hicho cha fedha


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X