Huwa inatokea mtu anaanza kitu unakikuza lakini inafikia hatua ambapo unapata anguko na kurudi chini. Kuna sababu nyingi zinazoweza kusababisha kuanguka, ikiwa ni pamoja na kupumzika kwa nguvu baada ya kuwa umefika juu. Au inaweza kutokana na sababu kuwa mwanzoni ulikuwa na lengo kubwa, ila baada ya kuwa umefikia juu au baada ya kuwa umefikia hilo lengo, sasa umekosa lengo kubwa zaidi.
Unakuta labda mtu ana lengo la kujenga nyumba, na kuitunza familia yake. Anapambana, anafikia hatua ambapo anapata hela ya kutosha kumwezesha yeye kujenga na kuitunza, sasa mtu huyu unakuta analala na kujisahau, sasa kitu hiki, na mwingine ni ile hali ya kupokea fedha nyingi kwa wakati mmoja. Anakuwa hajui namna ya kuzitunza na kuzitumia vizuri, anazitumia hovyo, mwisho wa siku, anaingia mkenge.
Sasa leo nataka nikueleze ni kwa namna gani unaweza kuanza upya baada ya kuanguka.
Lakini kabla sijakwambia hiyo, nataka nikwambie hauko peke yako. Kiuhalisia ni kwamba watu wengi huwa wanaanguka. Hakuna mtu ambaye huwa anaanzisha kitu na kukifanikisha moja kwa moja bila kupitia anguko lolote. Laiti kama maisha yangekuwa hivi, basi ni wazi kuwa kila mmoja angekuwa amefanikiwa sana.
Maisha ni kama huwa yana tabia ya kumjaribu mtu kuona kweli huyo mtu yuko siriazi na mafanikio anayoyataka? Yupo siriazi kweli. Na hapo ndipo kushindwa hutokea, ila kushindwa kwa kawaida siyo kushindwa, kushindwa ni fursa.
Leo hii nataka nikuoneshe namna gani unaweza kuanza upya baada ya kuwa umeanguka.
Kitu cha kwanza kabisa kama umeanguka ni wewe kujua kwa nini umeanguka. Jiulize, hivi imekuwaje mpaka nimeanguka wakati nilikuwa juu kabisa. halafu hizo sababu zitunze vizuri ili zisije zikakuangusha tena baadaye, maana ukifuatilia, vitu ambavyo huwa vinawaangusha watu ni vile vile. Hivyo, ukijua kilichokuangusha wewe, hata ukianza upya utakiepuka.
pili, kama umeanguka, hakikisha sasa unaweka mipango mipya ya kule unapotaka kwenda. Anzia palepale ulipo. Kisha endelea kusonga mbele. Unaweza kufika unapotaka na hata zaidi ya hapo. ubora ni kwamba kama ulishawahi kufika juu ukaanguka, unajua mchakato wote wa kufika huko. Na zamu hii itakuchukua muda kidogo zaidi maana mbali ya kuwa unaanzia chini, ila kuna baadhi ya vitu ulishavijenga tanagu mwanzoni ambavyo utavitumia sasa. mfano, vitu kama konekisheni, hata kama ulianguka, haimaanishi kuwa na konekisheni zako zote zilianguka. Kuna konekisheni ulizonazo sasa hivi, ambazo unaweza kuanza kutumia ili kusonga mbele.
Tatu penda kujifunza. unapaswa kuzama zaidi kwenye kujifunza ili upate maarifa yatakayokusaidia wewe kuinuka na kusongambele. Kama ambavyo nilikudokeza ni kuwa makosa ambayo watu wanafanya na kuwaangusha siyo kwamba ni mapya, ni makosa ambayo yamekuwa yakifanyika enzi na enzi, tokea enzi za mababu zetu. Ila tatizo ni kwamba watu hatujifunzi.
Mfano kama mahusiano yako yanaenda vibaya, haimaanishi kwamba, hilo tatizo linalokukumba wewe ni la kipekee na halijawahi kutokea hapa duniani, unachopaswa kujua ni kuwa limewahi kutokea na kuna watu wengine wamewahi kupitia kwenye hali mbaya zaidi ya kimahusiano kuliko hata wewe hapo. ila waliweza kutatua hiyo changamoto.
Tatizo lako ni kwamba hujifunzi na hupendi kusoma vitabu. na ndio maana unaendelea kurudia makosa yaleyale waliyofanya wengine, na kitu hiki kitakufanya uendelee kuanguka zaidi. Penda sana kujifunza.
Jifunze kuhusu biashara
Jifunze kuhusu mahusiano
Jifunze kuhusu fedha na mambo mengine ambayo unaweza kujifunza.
Kuanguka chini siyo tiketi ya wewe kutojifunza au kuwekeza kwenye vitabu. kuanguka chini kunapaswa kuwa ni tiketi yako ya kuanza upya, na tena zamu hii ukianza upya unapaswa ukue bila kurudi nyuma mpaka watu washangae.
Nne, jenga utaratibu wa kujifanyia tathimini kila mwezi , kila wiki na kila siku. Jiulize, hivi kweli nazidi kusongambele au ndio narudi nyuma. Kutojifanyia tathimini kunaweza kukufanya uanguke chini, kwa sababu kila mara utakuwa unajiona kama uanafanya vitu vinaenda sawa, ila kumbe kuna sehemu unakosea. Unaona ee. Hivyo, kila mara jiulize hivi kweli nipo kwenye njia sahihi? Hivi ni kweli nazidi kusongambele kama ninavyostahili au ndio narudi nyuma?
Jifanyie tathimini mara kwa mara.
Hii itakusaidia kwanza kuwekeza vitu na nguvu zako kwenye vitu vichache unavyoweza kufanya kwa ustadi.
NB. Tumeanza kusambaza vitabu vya jinsi ya kufikia ndoto zako. nakala ngumu (hardcopy). Kitabu hiki kinatumwa popote pale ulipo Afrika Mashariki. Hakikisha unapata nakala yako leo hii kwa bei ya punguzo. Yaani badala ya 20,000/- unapata nakala yako kwa 15,000/- tu. Mwisho wa kupata kitabu kwa bei ya oda ni tarehe 20. Jionee mwenyewe chini hapa muda uliobaki kupata nakala kwa bei hiyo hapo chini
[wpcdt-countdown id=”5798″]
Umekuwa nami,
Godius Rweyongeza
0755848391
Kwa maoni, ushauri au maswali: godiusrweyongeza1@gmail.com au info@songambele.co.tz
For bookings: songambele.smb@gmail.com au songambele@songambele.co.tz