KUNa wakati unahitaji upoteze kitu ili uweze kupata kitu. Kama haupo tayari kupoteza usitegemee kuokota.
Kama hauko tayari kupoteza mbegu za mahindi, usitegemee kwamba unaenda kuvuna mahindi.
Nadhani hii inaenda vizuri na ule usemi wa kihenga unaosema kwamba mtaka cha uvunguni sharti ainame. Au ule usemi wa kuwa mficha uchi hazai
Sasa swali ni kwako ni kitu gani upo tayari kupoteza kwa sasa ili uweze kunufaika kwa hapo baadaye.