Kwa watu wengi akitajwa kiongozi au mtu yeyote yule anayeitwa kiongozi basi wanafikiria kwamba kiongozi ni mtu mwenye cheo. Kama rais, waziri, mkurugenzi au cheo chochote kikubwa.
Kama hauna cheo wewe siyo kiongozi. Ninachoweza kusema hapa ni kwamba watu wanachanganya kati ya cheo na uongozi. unaweza ukawa na cheo ila ukawa siyo kiongozi. Na unaweza ukawa usiwe na cheo ila ukawa ni kiongozi.
Kwa hiyo sasa kiongozi ni nani?
Kiufupi ni kwamba kila mtu anapaswa kuwa kiongozi. Kiongozi wa maisha yake mwenyewe. Na sifa moja kubwa ya kiongozi ni kujisimamia. Hivyo, kama wewe unaweza kujisimamia na kufanya majukumu yako bila ya kuhitaji kusimamiwa basi ujue kwamba wewe ni kiongozi.
Kama hujaweza kujisimamia kwenye baadhi ya majukumu ambayo unafanya, basi ujue kwamba unapaswa kubadilika ili uanze kujijengea sifa za kuwa kiongozi.
Kuna vitu unaweza kuanza kukjisimamia kuanzia leo hii na vikakufanya kuwa kiongozi.
Kwa mfano huhitaji kuwa kiongozi ili kuamka asubuhi na mapema.
Huhitaji kuwa kiongozi ili uweze kusema ukweli na kuwa mwaminifu.
Huhitaji kuwa kiongozi ili uweke akiba
Huhitaji kuwa kiongozi ili ufanye kazi kwa bidii
Na hizo ni baadhi ya sifa ambazo kiongozi anapaswa kuwa nazo, na wewe huhitaji kuwa hata kiongozi ili uwe na hizo sifa.
umeshapata kitabu cha JINSI YA KUFIKIA NDOTO ZAKO?
kama bado, basi jipatie nakala yako sasa hivi, wasiliana na 0755848391