Kuna Nini Kwenye Toleo La Pili La Kitabu Cha Jinsi Ya Kufikia Ndoto Zako


Jana nilitangaza kuwa tarehe 20 Mei toleo la pili la kitabu cha JINSI YA KUFIKIA NDOTO ZAKO litakuwa tayari. Nakala zitafikishwa mpaka nyumbani kwako au ofisini kwako kwa wakazi mikoa ya Dar, Pwani na Morogoro. Hata hivyo, kama upo nje ya hii, mikoa, nakala zitatumwa na utazipokea vizuri tu. Nakala moja ni 20,000/- . hata hivyo, ukiweka oda ya kitabu sasa hivi utaweza kukipata kitabu kwa elfu kumi na tano. Hivyo, utaokoa elfu tano nzima.

Sasa unaweza kuwa unajiuliza kuwa kuna nini kwenye toleo hili la pili na kwa nini napaswa kusoma toleo la pili? Kwa nini eti?

Hapa sasa naenda kukupitisha kwenye toleo la pili kwa ufupi.

Nakumbuka mara tu baada ya kutoa toleo la kwanza, kitabu kilianza kusomwa na watu mbalimbali. Na muda huohuo nilianza kupokea mrejesho kuhusiana na kitabu kilivyokuwa kikisaidia watu. Asilimia kubwa ya watu waliosoma kitabu hiki walinipa mrejesho (sio wote).

Hivyo, nilichofanya kwenye toleo hili la pili, baada ya kuwasiliana na wale waliotoa shuhuda zao kuhusu kitabu, nimehusisha baadhi ya hizo shuhuda. Sijaweka nyingi sana, ila kuna shuhuda za kweli chache kutoka kwa wasomaji wangu wa toleo la kwanza.

Pili, kuna ongezeko la sura mbili mpya ambazo hazikuwepo mwanzoni. Ikumbukwe kuwa mwanzoni kitabu kilikuwa na sehemu tatu. Huku kikiwa na sura kumi na sita. Kwenye toleo hili jipya, kuna ongezeko la sura mbili mpya. kitu ambacho kinafanya kitabu sasa kiwe na sura 18. Kitabu kimeendelea kuwa na sehemu tatu, ila zenye sura 18.

Tatu, kuna marekebisho na vitu vichache Ila vyenye nguvu vimeongezwa karibia kwenye kila sura ya zamani. Na hivyo kufanya sura zote ziwe updated zaidi kuendana matakwa ya sasa.

Hili ndilo toleo la pili la kitabu cha JINSI YA KUFIKIA NDOTO ZAKO. Na sasa unaweza kuweka oda yako. Badala ya elfu ishirini (20,000/-) unaenda kupata kitabu hiki kwa shilingi 15,000

Weka oda yako sasa hivi kwa kuandika jina lako hapa. chini au kutuma ujumbe wenye jina lako sehemu ulipo kupitia namba hii 0755848391

Andika jina lako hapa chini (au nitumie ujumbe kwa 0755848391)

Sitaki ukose nakala hii ya kipekee sana. hivyo, jiweke kwenye orodha ya wale watakaopokea nakala hii ya kipekee kwa elfu 15,000/- tu badala ya 20,000/-

Andika jina lako hapa chini

1. Godius Rweyongeza 0755848391 (Morogoro Mjini-Morogoro)

2.

3.

4.

5.

6.

7.

8.

9.

10.

11.


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X