MAISHA YA NYOTA TANO


Leo nimesikiliza audiobook ya kitabu cha Oprah Winfrey. Nimejifunza mengi sana ila hapa kuna kimoja tu ambacho ningependa na wewe ukijue.
Oprah anasema kwamba, unaweza kuishi maisha ya nyota tano hata   hauna pesa sasa. Sio lazima ulale kwenye hoteli zenye viyoyozi ndio uanze kuishi maisha ya aina hii. Ebu ona

ukiamka asubuhi na mapema. Basi jipe nyota tano kwa ushindi huo.

ukitoka nje ukavuta pumzi na kufanya tafakari pamoja na kunywa maji. Jipe nyota tano kwa kitu hicho kikubwa.

Ukisoma kitabu, kurasa kadhaa, jipe nyota tano, maana hilo ni jambo kubwa.

ukiwahi kazini, jipe nyota tano pia.

ukimpigia ndugu, mke, mme, mzazi simu na mkaongea hadi mkacheka kiasi unasikia kichwa kama kinauma. hiyo ishara ya wewe kupata nyota tano kwenye hilo.

Yaani kiufupi ni kwamba. Maisha ya kila siku ukiyaishi vizuri sana. Basi utakuwa unaishi maisha ya nyota tano.

Bila shaka utakuwa umeona ilivyo rahisi kuishi maisha ya nyota tano.

Je, wewe leo umeishi maisha ya nyota tano?

Nashauri usome au usikilize audiobook ya kitabu hiki hapa. imebeba mambo mazito na muhimu kwa maisha yako.

kila la kheri.

Kitabu kinaitwa WHAT I KNOW FOR SURE.
Mwandishi Oprah Winfrey

makala hii imeandikwa na Godius Rweyongeza.
Tembelea pia www.songambeleblog.blogspot.com

kuna makala nzuri mimeweka.

kwenye youtube pia usikose kuangalia video hii. https://youtu.be/LrBROehGr64

nyingine zaidi zinakuja.
cha kufanya wewe SUBSCRIBE ili uwe wa kwanza kupata video hizi

haya twende https://youtu.be/LrBROehGr64


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X