Leo nimemkumbuka jamaa mmoja niliyesoma naye shule ya msingi na baadaye sekondari. Huyu jamaa alikuwa anapenda maisha mazuri sana, ila alikuwa hataki kufanya kazi ili kuyapata hayo maisha mazuri.
Alikuwa anapenda kufanya kazi kwenye ofisi nzuri ila alikuwa hapendi kupitia kwenye ule mchakato wa kumfikisha kwenye hiyo ngazi. Hivi kweli kitu kama hiki kinawezekana kweli
Yaani, itokee tu siku moja upo kwenye gari unaendeshwa kwenda kazini. unafika ofisini watu wanakuita bosi, bosi, bosi. Unasaini tu na kuondoka bila kufanya kitu chochote…Linawezekana hili kweli…
Sidhani hata kama mabosi wenyewe wanafanya hivi..
Kanuni ya asili ni kwamba, ili upate vinono, sharti ukubali kuvilipia gharama.
Mtaka cha uvunguni sharti ainame.
Huwezi kutaka kuishi maisha mazuri, wakati wewe mwenyewe Kwa hiyo, ondoa huo mtazamo wako uliokuwa nao.
- jua kitu unachotaka kwenye maisha, ila sasa kuwa tayari kulipa gharama ili uweze kukifikia.
- fanya kazi kwa bidii. Waru wanaweza kukushind kwenye vitu vingine vyote. Wanaweza kukushinda kwenye kipaji, watu wanaweza kukushinda kwenye kujituma, ila wasikushinde kwenye kuchapa kazi kwa bidii. Chapa kazi kwa bidii mpaka kieleweke
- Onesha kazi yako Haitoshi tu wewe kusema kwamba u mbunifu. Au kusema kwamba una kipaji, bila kuonesha kazi yako. Onesha kazi zako kwa watu. Watu wataziona hizo kazi, na hapo sasa ndipo wataamua kuwa wazichukue hizo kazi au la. Ila usichoke kuonesha kazi zako. Onesha kazi zako mara zote
- na kutokea hapo sasa, ndio siku moja utajikuta upo kwenye gari unaendeshwa, upo kwenye ofisi wenye kiyoyozi na mengine mengi.
Mimi nakuamini sana ila unapaswa pia kufanya kazi, ili hayo yote unayoyatamani yaje kwenye uhalisia.