Rafiki yangu wa ukweli Karibu kwenye makala ya jumapili ya leo. Leo ninataka nikwambie kwa nini unapaswa kuandika kitabu chako kuanzia leo hii.
Naikumbuka siku za nyuma niliwahi kuandika (SABABU 18 Kwa Nini Tunaandika Vitabu na Tutaendelea Kuandika Vitabu, Na Kwa Nini Wewe Unapaswa Kuandika Cha Kwako)
Ninachofanya leo ni kukuongezea nyama kwenye kile ambacho nimewahi kuandika.
Na hapa ninasema kwamba, unapaswa kuandika kitabu chako kwa sababu kesho na kesho kutwa unaweza usiwe hapa duniani. Sasa kuandika kitabu kutakufanya uache ujumbe kwa watu wa Karibu yako ili wajue fikra zako, kile ulichokuwa unasimamia kwenye maisha, ulipotoka mpaka kufika ulipofika. Kwa hiyo, kwamwe usisite kuandika kitabu chako. Anza leo hii kuandika kitabu chako.
Nina hakika wewe babu yako angekuwa ameandika kitabu, leo hii ungekuwa unaenda kukitafuta kukisoma. Kwa hiyo, kama ambavyo wewe unatamani kujua kitu kuhusu historia ya wazazi wako, hivyohivyo, andika kitu uwaachie wanao na wajukuu wako.
Upo tayari kuandika kitabu chako? Karibu upate kitabu cha NGUVU YA VITU VIDOGO KUELEKEA MAFANIKIO MAKUBWA. Kitakusaidia sana wewe kuanza kuandika kidogokidogo mpaka kukikamilisha hatuahatua. Kwa mfano kwenye kitabu nimeeleza kuwa unaweza kuandika kitabu chako Kama unavyoandika SMS.
Ebu fikiria kwa siku unaandika na kujibu SMS ngapi? Kwa mwaka hizi SMS zikiuunganishwa ni sawa na kitabu chenye ukubwa kiasi gani?
Ukiangalia hili, utagundua kuwa kitabu chako kinaweza kuwa kikubwa kama utatumia mbinu hii tu.
Kitabu kimeeleza vitu vingine VIDOGO unavyoweza kutumia kwenye kuandika kitabu chako na kukiuza kwa mafanikio.
Karibu upate nakala yako. Gharama yake ni 20,000/- na unatumiwa popote ulipo.
Lakini pia nina kitabu cha JINSI YA KUWA MWANDISHI MBOBEVU NDANI YA SIKU 30. Hiki nacho kinakuhusu pia. Kwa Sasa hiki kitabu kinapatikana kwa 5,000/- tu kwa mfumo wa softcopy. Karibu sana tuko pamoja.
Kupata vitabu hivi wasiliana na 0755848391.
Kila la kheri.
kwa maoni, Ushauri na maswali: godiusrweyongeza1@gmail.com
for booking: songambele.smb@gmail.com
One response to “Sababu Moja Kwa Nini unapaswa kuandika kitabu chako Leo”
Asante sana