Songambele


 
Rafiki yangu, muda wote na mara zote unapaswa kuwa mtu wa kusonga mbele. Usikubali kukwama na wala kubaki eneo lile bila ya kusongambele.

Vitu ambavyo vinakaa sehemu moja bila ya kusongambele huwa vina sifa mbaya kweli.
Maji yaliyotuama, ndio huwa yanazalisha mbu wa malaria. Hata mdomo wako ukiufunga bila kuongea kwa muda mrefu unatoa harufu mbaya.

Kwa kawaida asili haipendi kitu kikae bila ya kuwa kwenye mwendo. Ndio maana dunia linajizungusha kwenye mhilimi wake kila sekunde, matokeo yake ni usiku na mchana pamoja na majira (kiangazi, vuli, kipupwe..)
Ardhi ikikaa bila ya kupandwa kitu, utakuta kwamba ndani yake yanaota majani (magugu)
Hata watalaam wa afya hawashauri ukae eneo moja bila kuzunguka na kule.
 
Kwa hiyo, mara zote jiulize unapiga hatua? Unafanya  kitu cha kukufanya usonge mbele.
Usikubali kubaki eneo moja ukiwa umetuama kama maji…songambele la sivyo utazalisha mbu wa malaria.

Waingereza nao wana usemi wao, unaosema kwamba the idle  mind is the devils workshop. Ukimaanisha kuwa akili inayokaa bure ni karakakana ya shetani.

Sasa wewe unataka akili yako ichezewe na shetani..ukiona unakaa bila ya kufanya kitu, ujue kwamba unakaribisha shetani. Kwa hiyo badala yake songambele.
 
Nipo najiuliza ni kitu gani kinakuzuia wewe kusonga mbele? Je, ni kwa sababu huna mtaji? Je, ni kwa sababu ni kwa sababu unajiuliza kuhusu wazo lako la biashara ni bora au siyo?
 
JIFUNZE ZAIDI: USIISHIE TU KUKAA KWENYE KOCHI NA KUSEMA ONE DAY YES

Kumaliza tatizo hilo, nimekuandalia ofa ya vitabu vitatu kwa gharama ya elfu 12,000 tu. Hii ni ofa ambayo nadhani itakuwa ya mwisho mwisho kwa mwaka huu. siriaz! Unaweza usipate ofa nyingine kutoka kwangu mpaka mwaka huu unaisha. Kwa hiyo cha kufanya, ni wewe kuhakikisha kwamba unaichangamkia.
Tuma 12,000/- leo nikutumie ebooks tatu ambazo

MITAJI 8 ILIYOKUZUNGUKA NA JINSI YA KUITUMIA

NGUVU YA WAZO (the Powe Of An Idea): Jinsi wazo linavyoweza kubadili dunia pamoja na

KIPAJI NI DHAHABU: Jinsi ya kukigundua, kukinoa na kutumia kipaji chako.

Hizi ni ebooks tatu za kipekee sana kutoka kwangu ambazo zenye thamani kubwa sana ambazo unaenda kupata kwa bei ya ofa. Nadhani hii inaweza kuwa miongoni mwa ofa zangu za mwisho kabisa kwa mwaka huu. ichangamkie sasa…
 
Mpaka wakati mwingine, mimi ni Godius Rweyongeza kutoka SONGAMBELE
0755848391
Morogoro-Tz


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X