Habari ya leo. Siku ya leo ningependa kujibu swali la mtu mmoj amabye amesoma kitabu changu cha MAAJABU YA KUWEKEZA KWENYE HISA, HATIFUNGANI NA VIPANDE.
Anauliza swali hivi, samahani kuna kitu sijakikujua hapo, tofauti kati thamani yahisa na bei ya hisa
Kwa hiyo hapa kitu cha kujibu ni je, thamani ni nini? na bei ni kitu gani?
kwa kawaida thamani ya hisa huwa ni sawa ni bei ya ya hisa ya wakati husika. Kwa hiyo, kama hisa zinauzwa kwa shilingi 500, hiyo ndiyo itakuwa thamani yake pia.
Kitu hiki pia ndio kinatumika kupima utajiri wa watu. kwa mfano ukisikia wanasema bilionea fulani ana utajiri wa bilioni kadhaa ni kulingana na bei ya hisa kwenye soko la hisa, ambayo ndio inatuletea thamani ya utajiri wake.
Kwa mfano, ukifuatilia orodha ya mtajiri hapa duniani. Utagundua kwamba utajiri wao unakuwa unapanda na kushuka kila mara. Kinachofanya utajiri wao ushuke au kupanda siyo kitu kingine bali ni kupanda na kushuka kwa hisa. Kadiri hisa zinavyopanda au kushuka bei, ndivyo utajiri wao unapanda na kushuka.
Hili suala la kupanda na kushuka kwa bei ya hisa huwa linatokana na jinsi watu wanavyonunua na kuuza hisa zao.
Ikumbukwe kuwa hisa ni bidhaa zilizo sokoni, kama zilizyo bidhaa nyingine. Tuchukulie mfano wa kawaida tu wa nyanya sokoni. Kuna kipindi nyanya zinakuwa adimu na hivyo bei yake inakuwa juu. Na kuna kipindi nyanya zinakuwa nyingi sokoni na hivyo bei yake inakuwa chini. Hivyohivyo, kwenye suala zima la hisa.
Kupanda na kushuka kwake huwa kunategemea na jinsi ambavyo watu wanauza na kununua. Wanunuaji wakiwa wengi, maana yake kuna uhitaji, hivyo ambavyo thamani ya hisa itapanda na kadiri wauzaji wanavyokuwa wengi maana yake uhitaji ni mdogo na thamani ya hisa inashuka.
Thamani halisi ya hisa.
Hizo thamani za hisa zote huwa zinatokana na mihemko ya wanunuaji. Maana yake, watu ndio wanaweza kufanya thamani ya hisa ipande au kushuka. Hata hivyo, ukitaka kujua thamani halisi kabisa ya hisa unapaswa kutumia taarifa za ndani ya biashara.
Na yenyewe inapatikana kwa kuchukua rasilimali zote za kampuni kisha unatoa madeni yote ambayo kampuni inadaiwa, halafu unagawa kwa idadi ya hisa zote zilizo sokoni.
Thamani ya hisa =Rasilimali zote za kampuni (thamani kwa shilingi au dola)- madeni yote ya kampuni ÷ Idadi ya hisa zote zilizo sokoni
Kama kampuni tayari imeshaingia kwenye soko la hisa, taarifa hizi unaweza kuzipata kwa kufuatilia taarifa zake za mwaka au mhura husika.
Kama ndio inaingia mara ya kwanza kwenye soko la hisa utazipata kwenye ripoti yake inayotolewa kwa umma. Hata hivyo, utafiti binafsi unahitajika kwenye hili.
Kama bado hujasoma kitabu changu cha MAAJABU YA KUWEKEZA KWENYE HISA, HATIFUNGANI NA VIPANDE, nashauri sana usome kitabu hiki.
Kitabu kingine cha nyongeza ni kitabu cha NGUVU YA VITU VIDOGO KUELEKEA MAFANIKIO MAKUBWA
Unaweza kupata vitabu hivi kwa kuwasiliana na 0755848391
Fanya hivyo sasa hivi.
Umekuwa nami
Godius Rweyongeza
0755848391
Morogoro-Tz
Kwa maswali, maoni au booking: songambele.smb@songambele
One response to “Tofauti Ya Thamani Ya Hisa Na Bei Ya Hisa”
Asante sana umemjibu vizuri na ikawa darasa zuri sana