Uchambuzi wa kitabu cha Think And Grow Rich (Mambo 50 Ya Kujifunza)


Kitabu: THINK AND GROW RICH
Mwandishi: Napoleon Hill
Mchambuzi: Hillary Mrosso

Kupata kitabu cha THINK AND GROW RICH BONYEZA HAPA

Whatever your mind can conceive and believe it can achieve.

  1. Mafanikio yote yanaanzia kwenye mawazo, na ukiyaamini mawazo yako na kuyafanyia kazi utayaona mafanikio yako.
  2. Mafanikio mara zote yanakuja kwa wale wanaofikiria mafanikio kwenye fikra zao au mawazo yao.
  3. Mwandishi wa kitabu hiki ni Napoleon, ambaye inasemekana ndie mtu mwenye ushawishi zaidi kuwahi kutokea duniani, hasa kwenye masuala ya fedha, utajiri na biashara.
  4. Utajiri sio mara zote utapimwa kwa wingi wa fedha. Utajiri unajumuisha, afya njema, mahusiano mazuri, na mwenendo mzuri wa maisha.
  5. Ili kupata unachokitaka katika maisha unahitaji kuwa na matamanio dhabiti ndani yako, matamanio na tamaa kali ya kufanikiwa ndio itakusaidia kuchukua hatua.
  6. Unahitaji dhamira ya dhati kabisa na uvumilivu mkubwa ili kufikia na kuyaona mafanikio yako.
  7. Hakuna mafanikio yatakuja bila gharama za kuumia, kupoteza, kushindwa, kukataliwa au kuchukiwa.
  8. Unahitaji kuwa kinganganizi kweli ili kufikia malengo na mafanikio unayotaka, kifedha, kiuchumi, kifamilia nk.
  9. Katika safari yako ya mafanikio, unahitaji sana imani, mani itakusukuma na kukupa matumaini ya kuendelea mbele pale mambo yanapoonekana magumu.
  10. Imani ni muhimu sana katika safari ya mafanikio maana itakufanya uendelee kuamini ndoto zako na kuzipigania kwa uvumilivu.
  11. Katika kanuni na fomula za kufanikiwa kwenye maisha ya kifedha na kiuchumi ni kutokata tamaa, kamwe usikate tamaa kuufikia mafanikio yako.
  12. Kuwa na tamaa ya kupata mafanikio, penda kupata mafanikio unayoyataka na utayafikia licha ya changamoto zitakazojitokeza.
  13. Inawezakana kushindwa na kuambiwa haiwezekani mara moja au zaidi ya mara moja, kama ndani yako kuna ule moto na matamanio ya kufikia ndoto zako, endelea kuzifanyia kazi na kuzipigania.
  14. Kushindwa kwako jambo hakutafsiri kushindwa kwa wengine, au ndivyo itakavyokuwa kwa wengine.
  15. Kama umeshindwa wewe umeshindwa wewe, usitengeneze iwe sheria kuwa kwa kuwa wewe umeshindwa iwe hivyo kwa wengine kushindwa pia.
  16. Kumbuka siku zote wewe ndio mwamuzi wa hatima yako, maisha yako ya sasa na baadaye yanaathiriwa zaidi na wewe mwenyewe.
  17. Chukua hatua juu ya maisha yako, jipe jukumu la asilimia 100 la kuwajibika na maisha yako. Usimwachie mwingine maisha yako kama vile hayakuhusu.
  18. Tengeneza maisha bora unayoyataka na unayoyafurahia kuyaishi. Kuwa na mpango wa kila siku wa kuboresha maisha yako.
  19. Hakuna atakayeishi maisha yako badala yako, hakuna anayeweza kuyabadili maisha yako bila wewe mwenyewe kuamua, imiliki hatima yako.
  20. Amua mawazo yako yatawaliwe na hisia nzuri za mafanikio, utajiri, fedha na haki. Hayo yote yapo ndani ya uwezo wako kuyaruhusu na kuyatawala.
  21. Kumbuka pia unaweza kuruhusu mambo hasi na hisia za hofu, kushindwa, magonjwa na kukata tamaa vikatawala mawazo yako. Amua kwa dhati ni mambo gani unataka yatawale na yachukue sehemu kubwa ya fikra zako na mawazo yako.
  22. Chochote kitakachotawala mawazo, hisia na fikra zako kwa kiasi kikubwa hicho ndio kitakuwa rahisi kufanyiwa kazi na kutokea kwenye maisha yako, mfano kama ni fedha, utajiri, afya, Imani, upendo, chuki, hasira, vyote hivyo vinaweza kukaa ndani ya mawazo ya mtu na vina athiri mwenendo wake wote.
  23. Kama umeamua kulivalia njuga suala la mafanikio yako, basi fanya hivyo na jiweke kwenye msitari wa mbele kabisa wa mapambano ama ufanikiwe ama ukufe, kusiwe na uwezekano wowote wa kurudi nyuma au kukata tamaa. DO or DIE.
  24. Ukiamua kuingia kwenye njia ya mafanikio na kupata utajiri, akili, mwili, roho, nafsi na kila kitu ndani yako kinatakiwa kutambua jambo moja tu, ni kupambana hadi kufikia mafanikio hayo.
  25. Ondoa uwezekano wowote wa kurudi nyuma na kukata tamaa, kushindwa kunaweza kutokea lakini kukata tamaa hakutakiwi kutokea, pambana ufikie ndoto zako au ufe ukizipambania lakini sio kukata tamaa.
  26. Usitoe ruhusa kwa mawazo au akili yako kuleta hisia za kukata tamaa kwenye mapambano ya kufikia mafanikio yako ya kifedha, kielimu, kiuchumi au kiafya, pambana mpaka pumzi yako ya mwisho.
  27. Choma madaraja yote, ziba njia zote zitakazokufanya ufikirie kutoroka uwanja wa vita, salia uwanja wa vita ukipambania ndoto zako, hatima yako na uhai wako kwa nguvu zako zote.
  28. Weka mipango imara na madhubuti ya kufikia mafanikio yako ambayo haitajali utashindwa mara ngapi ili kufikia ndoto zako.
  29. Panga na weka mipango ya kuvumilia na kuendelea kung’ang’ania kubakia katika njia ya mafanikio yako.
  30. Kutamani tu hakutakuletea matokeo, panga, weka mikakati na fanyia kazi mipango hiyo hadi ilete matokeo uliyotamani, fanyia kazi matamanio yako.
  31. Matamanio yako ni vizuri yakachanganyika na imani na hisia kali za kukufanya uchukue hatua hata kama mazingira ni magumu, hata kama hakuna hamasa yoyote.
  32. Imani ina mchango mkubwa sana katika kutuletea utajiri, usipuuze imani katika safari yako ya mafanikio.
  33. Unajua hakuna ukomo kwenye fahamu zetu, isipokuwa ukomo tuliojiwekea wenyewe. Jipe ruhusa na ruhusu ufahamu wako kufikiri makubwa ili uchukue hatua kubwa zitakazo kuletea mafanikio makubwa.
  34. Utajiri na umasikini vyote vinaanzia au vinazalishwa na mawazo. Chagua mawazo unayotaka kazalisha katika fikra zako.
  35. Hakuna kinachoingia kwenye mawazo yetu bila sisi wenyewe kutoa ruhusa hiyo, toa ruhusa kwa mawazo chanya ya mafanikio kuingia katika fikra zako nafahamu zako.
  36. Maarifa pekee hayaleti utajiri wala fedha, kinacholeta utajiri na fedha ni matumizi ya maarifa uliyojifunza au kusikia. Fanyia kazi maarifa au elimu uliyoipata ili ilete matokeo.
  37. Onyesha maarifa yako kwa njia ya matendo, matendo yana nguvu na ushawishi zaidi, tekeleza unachojifunza.
  38. Maarifa bora hayataleta maisha bora kama huyatatekeleza. Uwe mtendaji wa neno usiwe msikiaji tu.
  39. Panga kabisa tena kwa kumaanisha kuwa utakachojifunza utakifanyia kazi, utaweka kwenye matendo unachojifunza, au maarifa unayopata.
  40. Thamani ya maarifa ipo pale unapoamua kuiweka kwenye matendo au kutekeleza. Jiahidi nafsi yako kuwa utaanza kufanyia kazi maarifa, ujuzi na elimu uliyoipata.
  41. Utofauti kwenye maisha unakuja pale unapoamua kufanyia kazi maarifa au elimu uliyoipata. Jitofautishe na wengine kwa kuwa mtendaji zaidi.
  42. Jifunze kila siku kuboresha ujuzi wako, pata maarifa ya kutosha kuhusu utalamu wako, itakufanikisha sana.
  43. Nidhamu ni muhimu sana katika safari ya mafanikio. Kama huna nidhamu huwezi kufika kwenye mafanikio yako.
  44. Nidhamu binafsi ndio kazi kubwa ambayo itakugharimu sana kuifanya.
  45. Tunahitaji nidhamu kwenye kila eneo la maisha yetu, nidhamu ya fedha, nidhamu ya muda, nidhamu ya kuendelea kufanyia kazi malengo yetu.
  46. Moja ya kazi kubwa unatakiwa kuifanya kwenye maisha yako ni kujizuia, kujidhibiti, kujitawala na kujiweza. Kama utafanikiwa kujitawala na kujiweza, basi umefanikiwa.
  47. Sio vizuri kuwapa wengine jukumu la kukusimamia, kukudhibiti ili uwe na nidhamu, jipe wewe mwenyewe hili jukumu liwe ndio jukumu la maisha yako yote.
  48. Kabla hujaanza kusimamia na kuwaongoza watu wengine, jisimamie, jimiliki, na jiongoze wewe mwenyewe kwa mafanikio kwanza.
  49. Uhuru wa kweli upo pale unapoweza kujidhibiti, kujizuia na kujitawala. Utumwa ni pale unapokosa utawala na udhibiti kwenye maisha yako binafsi.
  50. Dhibiti na tawala kila eneo la maisha yako, kifedha, afya, hisia, mapenzi, kazi, chakula, nk. Ukiweza kudhibiti mambo hayo utakuwa na maisha huru yenye afya na furaha.

Kitabu hiki kina mambo mengi sana ya msingi kwa ajili ya kuboroesha maisha yetu, hakifai hata kuchambua maana kila kilichoandikwa ni mafunzo muhimu sana. Nashauri kila mtu akisome kitabu hiki ili aboreshe maisha yake na ya watu wengine. .


5 responses to “Uchambuzi wa kitabu cha Think And Grow Rich (Mambo 50 Ya Kujifunza)”

  1. Hakika ili ufanikiwe katka maisha na kufkia malengo yako kwa usahihi inabidi kujifunza na kusoma vitabu mbalimbali ili kupanuwa wigo wa uelewa katka maisha ya utafutaji

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X