usifurahie kuitwa mnyonge. Hivi umewahi kujiuliza unyonge wako uko wapi? Sasa kwa nini watu wanakuita mnyonge na muda mwingine wanasema kwamba, wanakutetea wewe. Sikiliza, pambana kwa hali yoyote ile kuhakikisha kwamba wewe hauwi mnyonge. Kwa asili ni kwamba vitu vinyonge huwa havidumu. Sisi wenyewe hatupendi tukae na vitu vinyonge. Mfugaji wa ng’ombe hawezi kukaa na ng’ombe mnyonge mwaka mzima anamlisha tu. lazima atamuuza au atamchinja.
Na kadiri ya sheria ya Darwin vitu vinyonge, havidumu. Huwa vinatoweka na kuisha kabisa, huku vitu ambavyo ni imara, vikizidi kudunda tu. sasa kazi ni kwako, kuhakikisha kwamba hauwi mnyonge kwenye kile unachofanya, badala yake unaamua kuwa ngangali.
Kama ni fedha,pambana kuhakikisha kwamba unakuwa nayo. Kama ni kazi pambana kuhakikisha
Rafiki yangu usikubali kuwa mnyonge.
Umekuwa nami,
Godius Rweyongeza
0755848391
Morogoro-Tz
Kwa maswali, maoni au ushauri: godiusrweyongeza1@gmail.com
For bookings: songambele.smb@gmail.com