Utapata Kile Unachotaka Kama Utawasaidia Watu Kiasi Cha Kutosha


Utapata kile unachotaka kama utawasaidia watu kiasi cha kutosha kupata kile wanachotaka-Zig Ziglar.

Ili wewe kupata kile ambacho unataka maishani unapaswa kuwa tayari kuwasaidia watu kupata kile wanachotaka wao. Kadiri unavyowasaidia watu kupata kile wanachotaka, ndivyo na wewe unakuwa kwenye njia ya kupata kile unachotaka. Kwa hiyo, kazi yako kubwa unayopaswa kufanya ni kutafuta kujua kitu ambacho watu wanataka, kisha kuwapatia hicho kitu tu. baasi.

Na hii ndiyo njia ambayo unaweza kutumia kutimiza ndoto kubwa. unaweza kuanza kidogo huku ukitafuta kuwapa watu kile kitu ambacho wao wanataka. Kisha kwa kutumia hicho kitu kidogo, ukaendelea kukikuza na kuifanyia kazi ndoto yako.

Kwa mfano unaweza kunzisha bishara yenye lengo la kuwasaidia watu, kisha kwa kutumia hiyo, watu wakakulipa.

watu watakulipa kwa kutatua tatizo lao ambalo wewe umetatua. kwa hiyo basi, kitu kikubwa unachopaswa kushughulika nacho kuanzia sasa hivi, ni wewe kuanza kutatua matatizo ya watu. tatua matatizo ya watu, fedha itafuata.


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X