Fanya Kitu Hiki Kimoja Tu Kwenye Biashara Yako (Funzo Kutoka Kwa Makampuni Makubwa Kama Google, Facebook Na Amazon)


Unaendeleaje rafiki yangu wa ukweli
Leo nataka tujifunze kitu kutoka kwenye mitandao mikubwa na makampuni makubwa unayoyafahamu.

Na kitu hiki ni Kutengeneza mazingira ya kuwafanya wateja watumie muda mwingi kwenye biashara yako.

Au kutengeneza (kuwa na) kitu ambacho kitawafanya watu wazidi kuja kwenye biashara yako kila mara.

Hapa tujifunze kwa mitandao mingine mikubwa. Kila mara inatengeneza teknolojia mpya kwa lengo la kukufanya utumie muda mwingi kwao…

Google
Facebook
YouTube
Instagram

Wanabuni vitu vipya kila mara wakilenga mtu atumie muda mwingi kwenye mitandao yao.

Wanachojua ni kwamba kadiri mtu anavyotumia muda mwingi kwenye mitandao yao, ndivyo MTU atashawishika kununua.

Hivyohivyo, kwenye biashara yako, kadiri mtu atakavyotumia muda mwingi kwenye mazingira ya biashara yako ndivyo anavyoshawishika kununua.

Unaweza ukawa hauna biashara Ila kipaji chako tu. Kadiri mtu atakavyotumia muda mwingi kufuatilia Ubunifu au vitu ulivyofanya kutokana na kipaji chako, ndivyo mtu huyo atashawishika kununua kutoka kwako.
Ndivyo MTU huyo atakuwa shabiki wako.
Ndivyo MTU huyo atakuongelea zaidi kwa wengine.

Sijui hapo unanielewa.

SOMA ZAIDI: Fursa iliyotengeneza mabilionea kwenye karne ya 21

Chukulia mfano wa kawaida tu wa wasanii. Wasanii wanaofanya vizuri Ni wale wanaobuni vitu vipya mara kwa mara na kuwafanya watu wazidi kuwafuatilia zaidi

Sasa kuanzia leo hii, Anza kuangalia ni kitu gani unaweza kuongeza kwenye biashara yako, kwenye kipaji chako, kwenye ujuzi wako, kwenye mtandao wako n.k. ambacho kitawafanya watu watumie muda mwingi kufuatilia kazi, biashara au chochote unachofanya.

Anza leo hii hata Kama ni kidogo. Kuweka kitu hiki kwenye vitendo kuna vitabu viwili ambavyo vinaweza kukushika mkono na kukupa mwongozo. Cha kwanza ni NGUVU YA VITU VIDOGO KUELEKEA MAFANIKIO MAKUBWA na Cha pili ni ZAMA ZIMEBADILIKA. Kupata vitabu hivi wasiliana na 0755848391 sasa.

Shukrani Sana kwa wale wanaofuatilia mafunzo yangu. Leo naomba kupokea pongezi kutoka kwa

Kama na wewe ungependa kupata mafunzo yangu kwa njia ya baruapepe ili na wewe unufaike Kama huyo, jaza taarifa zako hapa


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X