Hiki ni kitu ambacho unapaswa kukitafuta kwa nguvu zako zote


Ni kitu gani hiki….
Ni kutafuta kuwaelewa wengine kabla ya kutaka kueleweka.

Kwenye maongezi ya kila siku kila mtu huwa anapigana kuhakikisha kuwa anaeleweka kwenye kile anachofanya.

Hiki kitu tu huwa kinasababisha ubishi mkubwa. Ninachotaka kukwambia leo ni kwamba tafuta kuwaelewa wengine kwanza kabla wewe hujaeleweka. Hilo litakusaidia sana maana ukishajua upande mwingine unataka nini itakuwa rahisi kwako kuweza kuwasilisha hoja yako na kuongea nao  waweze kukubaliana na wewe.

Hilo ndilo Jambo la msingi na KUBWA Sana ambalo unapaswa kupambania kila mara. Maana watu wengi huwa wanapenda kueleweka wao kwanza wakiwa hawataki kuwaelewa wengine. Sikiliza, kama hujawaelewa wengine, hata ukishinda kwenye mjadala bado ushindi wako haitakuwa wa maana. Hivyo Mara zote tafuta kuelewa watu kwanza kabla ya kueleweka.


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X